Mess Ampa Ahadi David Beckham

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mess Ampa Ahadi David Beckham
Baada ya nyota wa zamani wa Manchester United na Real Madrid David Beckham kutangaza kuwa yupo mbioni kuanzisha klabu ya soka, nyota wa Barcelona Lionel Messi amempongeza.


Messi ametoa pongezi hizo kupitia video fupi ambapo pia amemwambia Beckham kuwa huenda miaka michche ijayo akaungana naye kuchezea klabu hiyo.

''Kwanza nikupongeze sana kwa hatua hiyo mpya unayoianzisha, naamini kila kitu kitakwenda sawa, na huwezi jua miaka michache ijayo naweza kupokea simu kwaajili ya kuchezea klabu hiyo'', ameeleza Messi katika video hiyo.

Hivi karibuni nyota huyo aliyekipiga na vilabu kadhaa ikiwemo AC Milan na PSG ameweka wazi kuwa tayari wazo lake la kuanzisha timu itakayoshiriki ligi kuu ya Marekani (MLS) ameshaanza kulifanyia kazi na makao makuu ya timu hiyo yatakuwa jijini Miami.

David Beckham ambaye ni raia wa Uingereza alicheza kwa mafanikio katika soka ngazi ya klabu kabla ya mwaka 2007 kutimkia nchini Marekani kwenye klabu ya LA Galaxy.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad