Vanessa Mdee Kuinufaisha Familia ya Mubaraka Mwishehe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Vanessa Mdee Kuinufaisha Familia ya Mubaraka Mwishehe
Msanii wa muziki anayefanya vizuri kwa wanawake Bongo, Vanessa Mdee amebainisha ngoma ya ‘Pumzi ya Mwisho’ kuwa ni moja ya ngoma anayoikubali katika albamu yake ya Monday Money ambayo ina kionjo cha ngoma ya marehemu Mubaraka Mwishehe iitwayo ‘Jogoo la Shamba’
Vanessa amebaisha  kuwa kabla ya kutoa ngoma hiyo ya ‘Pumzi ya Mwisho’ aliyowashirikisha marapper wakali Joh Makini na Cassper Nyovest alifika nyumbani kwa marehemu Mubaraka Mwishehe na kuonana na familia yake ili aombe idhini ya kutumia kionja katika ngoma ya nguli huyo wa muziki wa dance pia kuona familia hiyo itanufaika vipi na mauzo ya ngoma hiyo.

“Pumzi ya mwisho ni wimbo ninao upenda sana kwenye ulbum yangu ya #MondayMondays. Ni moja kati ya nyimbo zangu bora kwenye album. Sababu kubwa ya Mimi kuchagua beat ya huu mwimbo ni kionjo kimoja kutoka kwenye wimbo wa hayati MBARAKA MWINSHEHE #Legend kabla ya album kutoka nikaona ni vema kuwaona familia ya MBARAKA kwanza ili nipate idhini ya kuendelea na kazi hiyo na kuona watanufaika vipi kama familia kupitika huo wimbo. Nashukuru walinipokea vizuri sana na walitoa idhini yao kwa mikono miwili kabisa.,” ameandika Vanessa katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

Akaongeza “Nusu ya mauzo ya wimbo huu kwenye mitandao ya kidigitali yataenda kwenye familia ya Mzee Mwinshehe siku zote. Nisingeweza kukamilisha kazi hii bila mkono wa @s2kizzy producer, Sauti ya @CassperNvoyest kutoka #SouthAfricana Mwamba @johmakini asanteni sana. Kuna mengi tuliongea kuhusu mzee ya kusikitisha na kufurahisha pia unaweza kuona video yote ukiwa na #VeeMoneyApp inapatikana kwenye store zote #PlayStore na #AppStoreAsanteni sana #MoneyMondays#PumziYaMwisho.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad