Wanaonizungumzia Mabaya Siwezi Kuwachukia Mungu Ndio Anajua- Wastara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wanaonizungumzia Mabaya Siwezi Kuwachukia Mungu Ndio  Anajua- Wastara
Msanii wa filamu nchini Wastara Juma Sajuki ambaye sasa anasumbuliwa na maumivu ya mguu na mgongo amefunguka na kusema kuwa watu ambao wanazungumza mabaya juu yake hawezi kuwachukia ila yeye amemwachia Mungu ndiye ajuaye yote.

Wastara amesema hayo wakati akiongea na www.eatv.tv na kusema anawashukuru sana Watanzania na Rais Magufuli kwa moyo wao wa upendo na kujali matatizo yake kwani licha ya watu kumzungumzia kwa mabaya lakini bado wanaendelea kujitoa kwa msaada na kwenda kumuona jambo ambalo linazidi kumpa faraja.

"Nawashukuru na wao kwa changamoto wanayotoa kwa upande wangu nimeweza kujifunza kitu wakati wewe una tatizo lolote kuna watu hakuamini, inawezekana watu hao unaishi nao, unatembea nao au unawachukulia ni watu wema lakini mwisho wa siku wamevaa ngozi tu ya kondoo ndani yake wana mioyo ya chui. Kwa sababu mtu kusema anaumwa anaweza kuangaliwa na jamii nzima hivyo mtu yoyote anaweza kunitembelea na kunishuhudia sasa kivipi unaweza kuidanganya jamii.

Wastara aliongeza kuwa "Niseme tu wao waendelee kutoa changamoto kama ambavyo wameamua lakini wajue kwenye matatizo Mungu pia anahusika, anaweza kutoa mitihani, anaweza kukupima imani hivyo huwa hayaji kwa mtu mmoja leo yapo kwangu mimi lakini kesho yanaweza kumkuta mtu anayempenda yeye au yakamgusa huyo huyo mzungumzaji sijui atakuwa na wakati gani? Ila mimi namuachia Mungu yeye ndiye atajua atahukumu nini kwa watu ambao wanaongea 'negative' ila mimi siwezi kuwachukia ila naamini Mungu anajua fungu lao ni lipi" alisisitiza Wastara

Aidha Wastara amesema kuwa kwa sasa maandalizi yake ya safari kwenda kwenye matibabu yanaendelea vizuri na kama mambo yatakamilika huenda Jumapili ya tarehe 4 Februari 2018 ataanza safari kuelekea India kwa matibabu.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad