Yanga Yasaini Mkataba Mnono wa Mabilioni

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Yanga Yasaini Mkataba Mnono wa Mabilioni
Mabingwa wateteziwa ligi kuu Tanzania Bara Yanga, leo wamesaini mkataba wa miaka 3 na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo Macron wenye thamani ya bilioni mbili.


Katika mkataba huo uliosainiwa kwenye makao makuu ya klabu hiyo, Yanga itatoa haki zote za utengenezaji na usambazaji wa jezi zao huku pia nembo ya kampuni ya Macron itaanza kuonekana kwenye jezi za Yanga SC.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amewaonya wote wanaouza jezi za klabu hiyo bila kuwepo kwa makubaliano na watawachukulia hatua za kisheria kwasababu sasa yupo mwenye haki ya kufanya hivyo. Pia Mkwasa amewakaribisha wawekezaji zaidi ndani ya klabu hiyo.

Naye Mkurugenezi mtendaji wa kampuni hiyo hapa Tanzania Suleiman Karim amewahakikishia wana Yanga kuwa klabu hiyo itapata faida kupitia mauzo ya jezi orijino za klabu.

Kampuni ya Macron inafanya kazi katika nchi zaidi ya 16 duniani zikiwemo England, Italia na Ufaransa. Hivi karibuni kampuni hiyo iliingia mkatata wa miaka 2 na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wenye thamani ya milion 800.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad