Zitto Kabwe Ataja Viongozi Ambao Atawateua ikitokea Amekuwa Rais wa Tanzania

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mchana wa leo January 30, 2018 kwenye ukurasa wa mtandao wa Twitter wa Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe ameandika watu ambao atawateua kushika nyadhifa mbalimbali za serikali kama atakuwa Rais wa Tanzania.

Ameandika kuwa atamchagua Mwanaharakati Maria Tsehai Sarungi kuwa Balozi wa Umoja wa Taifa huku Kaimu wake akiwa Mwanzilishi wa Nyama Choma Festival Carol Ndosi.

Amewataja pia Mbunge wa  Arumeru Mashariki Joshua Nassari na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa ACT-Wazalendo Ado Shaibu kuwa atawachagua kuwa Mawaziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Ulinzi wa Jamii na Biashara za Umma).

Zitto pia amewataja Mbunge wa Tarime Esther Matiko kuwa Waziri wa TAMISEMI, na Mbunge wa Viti Maalumu (CHADEMA) mkoa wa Geita Upendo Peneza kushika nafasi ya Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Hata hivyo Zitto ameongeza kuwa ambaye atamteua kuwa Katibu Mkuu Kiongozi hamtaji jina lakini yeye mwenyewe anajijua.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Utachezaje Play station Babab Mzima..??? Huoni hata Haya....
    Umeme wa Mgao. Si bora ungechaji Kisimati foni Chako.... Hiko Ki Tekeno.
    Zitto Buberi Kabwe rweyaga UNASIKITISHA TENA SANA... SPDI YA NGOSHA IMEKUBWAGA CHINI PWAAA... PWAAAA

    ReplyDelete
  2. Jamani ... Picha inajieleza na Mazingira yanayo msibu Huyu Dogo.
    A Thousand words being described on the Above Picture.

    Dogo anahitaji Msaada tena Wa Dharura. Anakwenda Kubaya Inahitaji kuwahiwa. Haraka Sana.

    ReplyDelete
  3. Kuota Mchana kwa wewe siyo Mbaya.
    Lakini utamwangaliaje Nabii Tito kwani Dkt Shika ameshasepa
    Mpaka wewe uanze kumteua MariaTsehai manaake kwanza unteua washkaji wako wa Hapo kijiwe Dam Damu.

    Sawa Mwanangu... Unazidi kututia Uchungu kila tukikuona Unaunda Serikali za Masaa halafu siku nyingine na Mambo yake Mengine kabisa.. Fanya Urudi Kwenu na Uzuru Malalo ya Wahenga wenu labda utakua poa baadae Dogo... Manake hapo hata nguo naona umevaa ...lakini usipojiangalia shauli yako..

    ReplyDelete
  4. Zito Unajua kucheza Usolo??
    Tena Usolo hata Luku hai hitajiki. Tujulishe kama unaujua.
    NSSF zile za Kigamboni naona Jana unazikingia Kifua.... Magu yuko njiani atafika tu. Jipange Dogo..!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad