Hatimaye Rais wa FIFA Atua Bongo Alfajiri ya Leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hatimaye Rais wa FIFA Atua Bongo Alfajiri ya Leo
Hatimaye rais wa Shirikisho la mpira wa miguu duniani fifa, Gianni Infantino amewasili nchini majira ya saa 10 : 30 alfajiri ya kuamkia leo na kupokelewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa JK Nyerere.



Infantino atakuwa hapa nchini kwaajili ya mkutano mkuu wa mwaka wa FIFA unaotarajiwa kuanza leo Februari 22 katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere huku ukitegemewa kuhudhuriwa na wajumbe mbalimbali wa Shirikisho hilo.


Baada ya kuwa hapa nchini, Infantino ataonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Magufuli.

Mkutano huu wa viongozi wa FIFA na CAF umebeba ajenda mbalimbali  ikiwemo kujadili Maendeleo ya Soka la Wanawake, Maendeleo ya Soka la Vijana, Utaratibu wa kusaidia Vilabu vya soka pamoja na vipaumbele mbalimbali vya kukuza soka kwa nchi za Afrika.

Infantino anatarajiwa kuondoka nchini mara baada ya kumaliza mkutano wake na kushiriki chakula cha jioni.

Picha zikionyesha Rais huyo wa FIFA, Infantino akiwa sambamba na rais wa CAF pamoja na wajumbe

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad