Shigongo Ajipa Madaraka Ajiteua Kuwa Balozi wa Hospitali ya Muhimbili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Shigongo Ajipa Madaraka Ajiteua Kuwa Balozi wa Hospitali ya Muhimbili
Mjasiriamali, Mtunzi wa vitabu mashuhuri nchini Tanzania na mmiliki wa kampuni ya Global Publishers, Erick James Shigongo amefunguka na kujiteua mwenyewe kuwa balozi wa hospitali ya Muhimbili.


Shigongo amefikia maamuzi hayo baada ya kujionea mabadiliko makubwa katika utoaji huduma katika hospitali hiyo na kusema kuwa awali alikuwa anaichukia hospitali hiyo kutokana na mambo mbalimbali ya hovyo ambayo yalikuwa yakitokea kipindi cha nyuma kitu ambacho kwa sasa hakipo tena.

"Mimi Eric Shigongo James, Leo Februari 12, 2018, nimeamua kujiteua kuwa Balozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, iliyopo Muhimbili jijini Dar es Salaam. Uamuzi huu nimeufikia kwa hiari yangu, bila kushinikizwa wala kuteuliwa na mtu yeyote, kwa sababu sina chembe ya shaka kwamba huduma zinazotolewa na taasisi hii ni bora, za kimataifa na zinaliletea sifa kubwa taifa letu. Nakiri kwa kinywa changu, Mungu shahidi yangu, kuwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na vitengo vyake vyote, imebadilika! Kwa hili nimshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli kwa kufanikiwa kupandikiza uzalendo, uadilifu na nidhamu ya kazi ndani ya mioyo ya Watanzania"

Aidha Shigongo amemuomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuendelea kuisaidia hospitali hiyo ya Muhimbili kwa ruzuku na vitendea kazi ili izidi kutoa huduma bora zaidi na kuokoa maisha ya Watanzania.

"Nimuombe, kwa mikono yote miwili, aiwezeshe hospitali hii kwa ruzuku, vifaa vya kutendea kazi na motisha kwa wafanyakazi ili iendelee kuokoa maisha ya Watanzania ambao wengi walikuwa wakifa kwa magonjwa ambayo yaliweza kutibika tu katika mataifa ya nje na si hapa nyumbani, jambo ambalo kwa hivi sasa halipo tena; kwani magonjwa makubwa ya moyo yanatibiwa hapahapa nyumbani na madaktari wetu wa Kitanzania"

Mbali na hilo Shigongo aliweka wazi jambo kuu lililomfanya yeye mwenyewe kujiteua kuwa Balozi wa Muhimbili

"Niliyoyashuhudia ndugu zangu ndiyo yamenifanya niamue kujiteua mimi mwenyewe kuwa Balozi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete pamoja na Hospitali ya Muhimbili, ndugu zangu Muhimbili imebadilika, si ile ya zamani, madaktari wanafanya kazi zao vizuri, wauguzi wanahudumia kwa kauli nzuri, dawa zipo ilimradi uwe na kadi yako ya bima, hakuna mbu Muhimbili kama ilivyokuwa zamani"

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad