Waziri Kigwangalla Ataka Ulinzi Uimarishwe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Kigwangalla Ataka Ulinzi Uimarishwe
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameuagiza uongozi wa wakala TFS kujenga kituo cha ulinzi wa kudumu katika eneo la chanzo cha maji ya mto Zigi kilichopo ndani ya Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani ili kulinda chanzo hicho.


Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari  baada ya kutembelea eneo la chanzo hicho na kukuta uharibifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya wananchi wanaodaiwa kuchimba madini ya dhahabu katika eneo hilo la hifadhi ambapo ni kinyume cha sheria.

"Nimeagiza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania  (TFS) wajenge kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo hili, na waweke walinzi wetu wa kudumu hapa badala ya kutegemea kufanya patrol (doria) na kuondoka, kwa sababu eneo hili wananchi wanaamini lina madini ya dhahabu kwa hiyo kila siku wataendelea kuja kujaribu kuvuna dhahabu kutoka hapa", amesema Dkt. Kigwangalla.

Pamoja na hayo, Dkt. Kigwangalla ameendelea kwa kusema "kwa sababu sisi kazi yetu ni kuhifadhi maliasili ambayo tumepata kama urithi wa nchi yetu, niwahakikishie kwamba tutaimarisha ulinzi kwa kuanzisha kituo cha ulinzi hapa ili askari wawe wanabadilishana na kudhibiti kabisa uharibu ambao umekuwa ukifanyika, kwa sababu maji yanayotoka katika chanzo hiki yanakwenda kunywesha Muheza yenyewe na wilaya wa Tanga, tukiharibu hapa yatakosekana maji safi na salama".

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala huyo, Prof. Dos Santos Silayo amesema pamoja na eneo hilo kwa sasa kuwa linalindwa na askari wa Suma JKT watahakikisha ulinzi unakuwepo muda wote kwa kutekeleza agizo hilo la Waziri la kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu ili askari wawepo katika eneo hilo muda wote.

----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Safi sana nchi yetu imejaaliwa mazingira mazuri ya asili lakini uharibifu wa mazingira unaoendelea kufanywa na baadhi ya watu ni vitu vya hatari na kuogopesha zaidi. Chanzo cha maji hata kikiwa kidogo kiasi gani kinapaswa kulindwa kwa nguvu zote ili kiendelee kuwepo au hata kufanywa jitihada za makusudi kukilea ili kiwe kikubwa zaidi.

    ReplyDelete

Top Post Ad