RC Tanga Ataka Uchunguzi Ufanyike wa Chanzo cha MotoBweni la Wanafunzi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

RC Tanga Ataka Uchunguzi Ufanyike wa Chanzo cha MotoBweni la Wanafunzi
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela ametoa siku 14 kwa vyombo vya ulinzi na usalama Wilaya ya Korogwe mkoani humo kufanya uchunguzi na kutoa ripoti ya chanzo cha kuteketea kwa moto  bweni moja la shule ya wasichana Korogwe usiku wa Machi 4, 2018.

Akizungumza mara baada ya kutembelea shule hiyo leo Machi 5, 2018 Shigela amesema ni mapema kuzungumzia chanzo cha moto huo huku akivitaka vyombo hivyo kuanza uchunguzi ili kubaini chanzo pamoja na madhara yaliyojitokeza.

“Kulitokea tatizo la umeme kuwaka na kuzima ambalo hata mkoani lilikuwepo ila hatuna uhakika, hivyo naagiza vyombo vya ulinzi na usalama kwa siku 14 kuchunguza chanzo cha tatizo na athari zake kwa wanafunzi na mali zao ili tujue,” amesema Shigella

Pia, Shigela ameagiza wadau wa elimu kuona umuhimu wa kuchangia shule hiyo kwa maelezo kuwa yanahitajika magodoro na vifaa vingine muhimu shuleni hapo ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo yao.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo, Annisia Mauka amesema hakuna madhara kwa mwanafunzi yeyote kwani wakati moto unatokea wote walikuwa wanajisomea darasani.

Amesema mpaka sasa kuna bajeti ya Sh1.3bilioni kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo yakiwemo mabweni ila hakuna bajeti ya bati kwa ajili ya ujenzi.

Daktari wa Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, Frank James amesema walipokea wanafunzi 43 walioonekana wazi kuathiriwa na moshi wakati bweni hilo likiwaka moto lakini walipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurudi shuleni.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad