CAF Kuchunguzwa Watanzania kwa Kashfa ya Rushwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

CAF Kuchunguzwa  Watanzania kwa Kashfa ya RushwaShirikisho la soka Barani Afrika CAF linaendelea na uchunguzi juu ya tuhuma za kupanga matokeo (Match fixing) zinazowakabili waamuzi wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Taarifa ya TFF iliyotolewa leo na Kaimu katibu mkuu Kidao Wilfred imeeleza kuwa CAF imewajulisha TFF juu ya tuhuma hizo, zinazowahusu waamuzi wa mchezo wa Ligi ya mabingwa kati ya Rayon Sports ya Rwanda dhidi ya Lydia Ludic Burundi Académic FC ya Burundi.

Waamuzi wa Tanzania waliochezesha mchezo huo uliomalizika kwa Rayon kushinda 1-0  huko Burundi Februari 21, ni Mfalme Ally Nassoro, Frank John Komba, Sudi Idd na Israel Mkongo Mjuni ambaye alikuwa mwamuzi wa akiba.

CAF imeieleza TFF kuwa siku koja kabla ya mchezo viongozi wa timu ya Rayon wanadaiwa kufika hotelini walipokuwa waamuzi na kuingia kwenye vyumba vyao hivyo CAF inahitaji maelezo ya waamuzi kabla ya Machi 6.

Hata hivyo TFF imeweka wazi kuwa haina nia ya kumuonea mtu bali haki itatendeka na kama watabainika kuhusika wachukuliwa hatua kali. Rayon Sports ilisonga mbele baada ya kuwa imetoka sare nyumbani ya 1-1 hivyo kuwa na ushindi wa mabao 2-1.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad