Sakata la Daimond, Waziri Shonza Lamuibua Stara Thomas Ataka Wakutane Kuweka Mambo Sawa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sakata la Daimond, Waziri Shonza Lamuibua Stara Thomas Ataka Wakutane Kuweka Mambo Sawa
Msanii wa siku nyingi wa bongo fleva, Stara Thomas amesema anatamani msanii Naseeb Abdul ‘Diamond’ aliyeingia kwenye vita ya maneno hivi karibuni na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Juliana Shonza kukutana ili kuyaweka mambo sawa.



Wiki hii Shonza na Diamond wamejikuta katika vita ya maneno iliyosababishwa na kitendo cha kufungiwa kwa nyimbo 15 za baadhi ya wasanii ukiwemo wa Diamond wa Halleluya na Wakawaka.



Diamond amedai waziri huyo amekuwa akifanya mambo kwa kukurupuka kwa lengo la  kutafuta ‘kick’ kwenye vyombo vya habari au kuogopa kutumbuliwa.



Hata hivyo, Shonza amesema hayupo tayari kumjibu msanii huyo na kumtaka kufuata taratibu za kufika ofisini kwake au kuandika barua kama anaona hajatendewa haki badala ya kuzungumzia kwenye vyombo vya habari na mitandao, huku Diamond akisema kwa nini hakumwandikia barua kabla ya kumfungia.



Akizungumza na MCL Digital, Stara ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya maadili ya Chama cha Bongo Fleva (Tuma), amesema anajua Diamond alichokifanya si sahihi na alikuwa na hasira, wakati akitetea kile alichofanyiwa na kushauri kuwa ni wakati wake kukutana na waziri ili kuweka mambo sawa.



“Ifike mahali wasanii wajue kwamba huwezi hata siku moja ukashindana na Serikali hata kama unajiona hujakosa, zipo taratibu za kuweza kufuata kwa unacholalamikia na si kutumia lugha isiyo ya staha kwa kiongozi aliyepewa dhamana na Rais kusimamia sekta fulani,” amesema.



“Najua inaumiza wasanii tumekuwa tukipigania kazi zetu wenyewe na ndio maana hata mdogo wangu Diamond kajikuta anashindwa kuficha hasira zake, lakini hii kamwe haiwezi kumsaidia kwa sababu anashindana na mamlaka iliyopo juu kisheria.”



Kwa upande wa Serikali, amesema ni vyema ikawa na utaratibu wa kukutana mara kwa mara na wasanii kuwapa elimu ya mambo wanayotakiwa wayafanye na yapi hawatakiwi kuyafanya, jambo litakalowasaidia kuepuka kuingia nao katika migogoro ya aina hii.



Kuhusu kama tangu sakata hilo lianze kamati ya maadili ya bongo fleva imeshamuita Diamond, Stara amesema inakuwa vigumu kwa kuwa msanii huyo si mwanachama wao na kwamba, utaratibu wao ni kufanya hivyo kwa wanachama wao.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad