TFF Yamsaka Atakayechukua Mikoba ya Mayanja

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

TFF Yamsaka Atakayechukua Mikoba ya Mayanja
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeanika wazi vigezo vipya watakavyovizingatia mara baada ya kuanza rasmi kupitia ‘CV’ mbalimbali walizopokea zitakazowafanya kumpata kocha mpya atakayechukua mikoba ya kocha wa sasa, Salum Mayanga.



TFF inaingia katika mchakato wa kutafuta kocha mpya baada ya mkataba wa kocha wao wa sasa Mayanga kumalizika tangu mwezi uliopita, huku akiendelea kukitumikia kikosi hicho kwa maombi maalumu.



Akizungumza na Championi Ijumaa, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Wilfred Kidau, alisema pamoja na Mayanga kuendelea kuitumikia Stars kwenye michezo miwili ya kirafiki iliyopo kwenye kalenda ya Fifa, mkataba wake ulishamalizika, hivyo TFF tayari ipo katika mchakato wa kuhakikisha inampata kocha mpya ambaye atakuwa na vigezo vya kuifikisha Stars katika anga za juu.



“Uongozi kwa sasa umejipanga kikamilifu kuhakikisha soka letu linafika mbali na ndiyo maana utaona karibia michuano yote ya kimataifa vikosi vyetu vya taifa vinashiriki na TFF inafanya kila liwezekanalo ili tuweze kufuzu kwa kila hatua inayoendelea mara tu baada ya kuingia katika michuano yoyote iliyo mbele yetu.



“Lakini kama hilo halitoshi, TFF tumejipanga kuhakikisha tunampata kocha mwenye CV kubwa zaidi ya aliyepo na kama atakosekana mwenye vigezo vya kumzidi Mayanga basi hatutakuwa na haja ya kutafuta kocha mpya.

“Kwa kuwa walimu wapo wengi wenye viwango, itategemea na hao wanaopitia majina maana makocha ni wengi.



“Kama unavyojua mwingine anaweza akapatikana na asiwe tayari kuja bila maelewano na timu yake hivyo zoezi la kumtangaza litategemea na muda utakaotumika kukamilisha mambo yote hayo,” alisema Kidau.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad