Tunamchunguza Nondo Kama Kweli Alitekwa! – Jeshi la Polisi Iringa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Jeshi la Polisi Mkoani Iringa limefunguka na kuweka wazi kuwa mwanafunzi wa mwaka wa tatu UDSM, Adbul Nondo alifika kituo hicho cha polisi jana Machi 7, 2018 na kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana.

RPC mkoa wa Iringa, Juma Bwire amesema kuwa jeshi la polisi limefungua jalada la uchunguzi ili kubaini ukweli kama mwanafunzi huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania kama kweli alitekwa au la.

“Jeshi la polisi mkoa wa Iringa limefungua jalada la uchunguzi kubaini ukweli kama alikuwa ametekwa na kama alitekwa tunaaidi kwamba sisi jeshi la polisi likiwapata watuhumiwa sheria itachukua mkondo wake aidha tunaendelea kuchunguza kama ametoa taarifa za uongo kwa njia ovu kwa lengo la kutaka kuhamasisha wanafunzi wenzake ili kuleta uvunjifu wa amani nchini tutamshughulikia kama waalifu wengine”

Aidha RPC amesema kuwa mwanafunzi huyo kwa sasa anaendelea vizuri na wala hana majeraha yoyote yale kwani hajapigwa na ni mzima wa afya njema na kusema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo ili kujua nini kilimsibu.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania Abdul Nondo alipotea katika mazingira ya kutatanisha Machi 6, 2018 akiwa jijini Dar es Salaam majira ya saa tano usiku na kupatikana Mafinga Iringa Machi 7, 2018.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hakuna cha kutekwa wala ushuzi, kutaka sifa kutakuponza.

    ReplyDelete

Top Post Ad