Mbarawa Apangua Hoja za Wabunge....Asema Ndege Nyingine Kubwa ya 7 Itanunuliwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa jana amepangua hoja wa wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya wizara hiyo huku akithibitsha kuwa Serikali inatarajia kununua ndege nyingine kubwa ya saba ya masafa marefu.

Alisema Serikali haikurupuki kununua ndege hizo kwa kuwa inao mpango kazi unaobadilishwa kila mara kulingana na wakati.

“Serikali itaendelea kununua ndege na haitakodi kwa sababu kukodi ni gharama kubwa ikilinganishwa na kununua.

“Nia ya serikali ni nzuri kwani huwezi kuwa na viwanja vya ndege kama huna shirika lako la ndege, hivyo tumenunua ndege sita ambazo tatu zimetua na zinafanya kazi.

"Mwaka huu tunategemea ndege tatu zitawasilisha ambazo ni Boeng 787 ya masafa marefu yenye uwezo wa kuchukua abiria 262, nyingine mbili zenye uwezo wa kuchukua abiria 132 kila moja ni Bombardier CHCS 300 ambazo zitawasilia na kuanza kufanya kazi.

“Kikawaida huwezi kuwa na ndege moja ya masafa marefu ikafanya kazi vizuri hivyo kwenye bajeti hii tumeshapanga kununua ndege nyingine boeng 787 ili tuwe na ndege mbili za masafa marefu ambapo moja ikiwa inatoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou na moja inatoka Guangzhou kuja Dar es Salaam. Ndio utaratibu unavyokwenda,” amesema.

Aidha, amesema kwamba Kampuni ya Ndege (ATCL), inao mpango kazi hivyo si kweli kwamba haina kama wabunge walivyodai ambapo kila baada ya muda inabadilishwa kwani si msahafu hivyo itabadilishwa kutokana na mahitaji ya soko.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad