Ndege Kubwa Zaidi ya Emirates Iliyobeba Abiria 475 Yatua kwa Dharura Dar...

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ndege ya Emirates Iliyobeba Abiria 475 Yatua kwa Dharura Dar
Ndege ya kampuni ya Emirates iliyokuwa ikielekea Mauritius ikiwa na abiria 475 wakitokea Dubai, imetua jijini Dar es Salaam leo kwa dharura kutokana na hali mbaya ya hewa nchini humo.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege Tanzania, Kamishna msaidizi, Matanga Mbushi ameithibitishia MCL Digital, taarifa hizo akisema ndege hiyo ya Emirates, aina ya Airbus 380, EK701, ilishindwa kutua mara tatu nchini Mauritius kutokana na mvua kali iliyokuwa ikinyesha.

“Hiyo ndege ilikuwa ikielekea Mauritius, sasa hali ya hewa imekuwa mbaya ikashindwa kutua. Rubani alijaribu kutua mara tatu lakini akashindwa ndipo akaamua kuja Dar es Salaam kutua kwa dharura,” alisema Mbushi.

Amesema ndege hiyo ilikuwa na abiria 475 na wote wamepangiwa hoteli ili kusubiri taarifa za hali ya hewa ikiwa nzuri waendelee na safari.

“Kesho kama hali itakuwa nzuri wataondoka,” amesema Mbushi.

Ndege hiyo ni ya Shirika la Emirates la Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE). Ni kampuni tanzu ya Emirates Group, ambayo inamilikiwa na Shirika la Uwekezaji la Serikali ya Dubai.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad