Rais Magufuli Atumia Wimbo wa 'Hawawezi Kushindana' ya Goodluck Gozbert Kuwafikishia Ujumbe... Aomba Urudiwe Mara Mbili

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais Magufuli Atumia Wimbo wa 'Hawawezi Kushindana' ya Goodluck Gozbert Kuwafikishia Ujumbe... Aomba Urudiwe Mara Mbili
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameshindwa kujizuia na kuomba kupigiwa kwa mara ya pili wimbo wa msanii wa injili nchini Goodluck Gozbert, uitwao  'Hauwezi Kushindana'


Rais Magufuli ameweka wazi kuwa amevutiwa sana na wimbo huo wakati akiaanza kuhutubia leo April 3, 2018 katika uzinduzi wa mradi wa kuzalisha umeme Kinyerezi 2, ambao unatarajiwa kuingiza megawatts 240 katika gridi ya Taifa.

Baada ya kumaliza kuhutubia Rais Magufuli aliomba wimbo huo upigwe tena na kukiri kuwa amemkosha sana.

"Naomba niseme tena kale kawimbo kamenigusa sana, naomba kachezwe tena hapa " alisisitiza Rais John Pombe Magufuli

Msanii Goodluck Gozbert ameachia video ya wimbo wake huu Machi 16, 2018  na kuwagusa watui wengi kutokana na utunzi wake na ujumbe ambao upo ndani ya wimbo huo ambao pia umemguda Rais John Pombe Magufuli.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad