Sakata la Matibabu Lissu Amvaa Spika Ndugai "Bunge Linavunja Sheria Linaendeshwa kwa Chuki na Upendeleo wa Kisiasa"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sakata la Matibabu Lissu Amvaa Spika Ndugai "Bunge Linavunja Sheria Linaendeshwa  kwa Chuki na Upendeleo wa Kisiasa"
Mbunge Tundu Lissu amefunguka na kudai sheria ya uendeshaji wa Bunge halijaweka masharti yeyote ya kupatiwa fedha za matibabu kama alivyo tangaza Spika wa Bunge Job Ndugai hivi karibuni na wala hakuna kifungu chochote kinachozungumzia kibali cha Hospitali ya Muhimbili au cha Rais Magufuli.


Lissu amebainisha hayo usiku wa kuamkia leo kupitia ukurasa wa kijamii zikiwa zimepita takribani siku tatu tokea Spika wa Bunge, Job Ndugai kutoa ufafanuzi juu ya matibabu ya Mbunge huyo kuwa Bunge haliwezi kuidhinisha fedha kwa ajili ya matibabu yake kwa kuwa halijapata vibali vitatu ambavyo vingemuwezesha kupata fedha za matibabu kutoka Bungeni.

"Ukweli ni kwamba kauli ya Spika Ndugai inathibitisha jinsi ambavyo Bunge limepoteza mamlaka na hadhi yake chini ya uongozi wake dhaifu. Hata masuala ambayo Sheria haijampa Rais mamlaka, Spika Ndugai ameyakabidhi. Kauli hiyo ni uthibitisho pia wa jinsi ambavyo Bunge linaendeshwa bila kufuata sheria, kwa chuki na upendeleo wa kisiasa", amesema Lissu.

Pamoja na hayo, Lissu ameendelea kwa kusema "yeye amekwenda India mara nyingi kutibiwa kabla na baada ya kuwa Spika kwa gharama za Bunge. Mimi mbaya wao niliyepigwa risasi nikiwa nahudhuria vikao vya Bunge ninakataliwa matibabu kwa sababu zisizokuwa na msingi wowote. Sio kweli kwamba sikufuata utaratibu, kama maana ya neno hilo ni utaratibu uliowekwa na sheria".

Lissu ameendelea kusema..

"Kusema nisubiri kibali cha Bunge au cha Muhimbili au cha Rais Magufuli ilikuwa ni kunitakia kifo cha wazi.
Katika mazingira ya jaribio la mauaji dhidi yangu, utaratibu pekee uliokuwa unawezekana ulikuwa ni kunihamisha nchini kwa dharura. Nilikuwa nimeumizwa vibaya, mifupa imevunjwa kila mahali, nimepoteza damu nyingi na risasi zimejaa tumboni. Kusema nisubiri kibali cha Bunge au cha Muhimbili au cha Rais Magufuli ilikuwa ni kunitakia kifo cha wazi".

Aidha, Lissu amedai uamuzi wa yeye kupelekwa Nairobi nchini Kenya umetokana na makubaliano ya kikao kilichofanyika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma ambapo Spika Ndugai na Naibu wake walikuwepo kwenye kikao hicho pamoja na viongozi wengine wa nchi akiwemo Waziri wa Mambo ya Ndani Mwigulu Nchemba, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu na Katibu Mkuu wake Dkt. Ulisubisya Mpoki na Mwenyekiti Mbowe na wabunge kadhaa walihudhuria pia.

"Baada ya kukubaliana kwamba napelekwa Nairobi, ndege ililetwa Dodoma saa sita za usiku. Uwanja wa Ndege wa Dodoma hauruhusu ndege kuruka au kutua baada ya saa 12 jioni. Nani aliyeruhusu ndege iliyonichukua kutua na kuruka saa sita usiku kama hakukuwa na kibali cha Bunge?", amehoji Lissu.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kiukweli kabisa yeye Tundu Lisu muache apige kelele mpaka apasuke kwa masuala ya kibishi ndio taaluma yake lakini sheria ipo wazi hata kwa mtanzania asiekwnda shule anafahamu yakwamba ukitaka kwenda kutibiwa nje ya Tanzania lazima serikali kwa kupitia uthibitisho wa Hospital kuu ya Taifa kwamba unahitajika kwenda kutibiwa nje. Chadema kupitia viongozi wake walimpeleka Tundu Lisu Nairobi bila ya kushauriana na serikali kiasi kwamba hawakutaka serikali ijuhusishe na Masuala ya Lisu. Serikali kwa busara zake wakawaachia Chadema wafanye wanavyotaka kufanya kuhusiana na matibabu ya Lisu. Serikali kisheria ilikuwa inauwezo wa kuizuia Chadema kumpeleka Lisu Nairobi na kuchukua jukumu la kumuhudumia kimatibabu. Lakini fikiria kama serikali ingeamua kutumia nguvu kumchukua Lisu na kumuhudumia pale alipojeruhiwa? Sakata lake na Chadema lisingekuwa dogo na hapana shaka Chadema wangepata nafasi ya kuzusha kila aina ya uzushi ndio maana tunasema serikali imetumia busara. Ukiachilia mbali na Masuala yote hayo. Tundu Lisu licha yakuwa kweli kabisa ameumizwa vibaya na waliomuumiza wamewaumiza watanzania wengi lakini Kauli za Tundu Lisu juu ya serikali na Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati akiwa huko matibabuni zinatia kichefuchefu. Tundu Lisu ni m'binafsi asieitakia mema Tanzania na watanzania na kuulekeza Nguvu zake katika kujijali yeye tu hajali kuipaka taswira mbaya Tanzania katika jumuiya za kimataifa. Huwezi kumkomoa Magufuli au CCM kwa kuipaka matope Tanzania huko ni kuwakomoa watanzania na kamwe hatuungani na vitendo hivyo vya hovyo vya kisaliti.

    ReplyDelete

Top Post Ad