AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Yanga imefanikiwa kutinga katika hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kufanikiwa kuiondoa Wolaitta Dicha ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 2-1.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Julio alisema linapokuja suala la kitaifa utani uwekwe pembeni na watu wote waungane na kuwa kitu kimoja kwa lengo la kuusogeza mbele mpira wetu.
“Nimefurahi Yanga kuingia hatua ya makundi kwani imesaidia Tanzania kuendelea kusomeka katika ramani ya mpira, ukiangalia leo hii Tanzania tunasomeka kupitia wachezaji Samatta (Mbwana) na Msuva (Simon).
“Kwa hiyo kama wamepata nafasi hiyo ni fahari kwa Tanzania japokuwa kuna utani wao wa Simba na Yanga kwenye mitandao unaendelea ambao unaweza kuwa na faida au hasara kwa pande zote mbili. Kwa sasa tuangalie utaifa kwani itatusaidia.
“Utani wetu ubaki utani na linapokuja suala la kitaifa watu wote tuungane tuwe kitu kimoja na kuiunga mkono Yanga japokuwa kuna watu wengi wa Simba hawakupendezewa na hatua hiyo kufuatia utani wao wa Simba na Yanga,” alisema Juli
Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu
Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
Hicho kitu julio angekizumza wakati SIMBA inacheza na Almasry sio leo.
ReplyDelete