Video:Makonda Atema Cheche kwa Wabunge Wanaokosoa Kampeni Yake "Faragha Ukiwa Chumbani ila Ukiitwa Kimbia Usisubiri Nikufate"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makonda Atema Cheche kwa Wabunge Wanaokosoa Kampeni Yake "Faragha Ukiwa Chumbani
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema wale wote wanaosema kampeni yake ya kuwasaidia akina mama waliotelekezwa na watoto imevunja sheria, pengine wana watoto nje na wanaogopa kujitokeza.

Makonda ameyasema hayo leo Aprili 19, katika uzinduzi wa hospitali ya kisasa ya mama na mtoto iliyopo Chanika iliyojengwa kwa msaada wa Shirika Maendeleo la Kimataida la Korea (Koica).

“Eti wanasema navunja sheria, natakiwa nifanye faragha kama unataka faragha tunza mtoto. Mimi siogopi, nipo tayari kufungwa lakini kwa ajili wa kutetea haki za watoto. Pengine hao wanaosema navunja sheria wana watoto wao nje wanaogopa kujitokeza,” amesema.

Jana, Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi  akiwa bungeni alisema kampeni hiyo inaweza kuleta hali ya sintofahamu na akabainisha kuwa inapaswa kufanyika faragha na sio kama inavyofanyika sasa.

Awali, Waziri wa Afya, Jinsia, Wanawake na Watoto,  Ummy Mwalimu alisema kampeni hiyo ni sahihi ila kasoro yake ni kutokuwa na faragha, lakini akasema kwa sasa inafanyika huku picha za watoto zikifichwa.

Aliyeibua hilo bungeni jana alikuwa ni mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga aliyehoji uhalali wa kampeni hiyo na akahoji kama haivunji sheria na kuwavunjia haki wanawake na watoto.



-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hizo siri siri zisizo na mwisho matokeo yake ndo huo mlundikano wa umati wa wanawake waliotelekezwa na watoto. Enough is enough hatutaki tena utelekezwaji. Na NGO zianze mara kutoa elimu kwa akinamama kumsaidia mambo ya kuzingatia kabla ya kuamua kutengeneza familia.

    ReplyDelete

Top Post Ad