Wema Sepetu: Sioni Wivu Diamond Kumkumbatia Hamisa Mobeto

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wakati habari zilizopo mjini kwa sasa ni tukio la mwanamitindo Hamisa Mobetto na msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ’Diamond’ kuteka tukio la utoaji tuzo za filamu za Sinema Zetu International Film Festival Award (SZIFF), kwa mrembo Wema Sepetu yeye kaichukulia kawaida.

Diamond na Mobeto katika tuzo hizo zilizofanyika jana ukumbi wa Mlimani City , walikwenda kama wageni waalikwa, walichaguliwa kukabidhi tuzo kwa mshindi wa kipengele cha ‘Best Original Music’ ambayo ilikwenda kwa filamu ya Safari ya Gwalu.

Katika kipengele hicho watu walikuwa wanasubiri kwa hamu kuona namna gani Wema ataweza kukabidhiwa tuzo na wawili hao, kwa kuwa filamu yake ya ‘Heaven Sent’ ilikuwa ni mojawapo iliyokuwa ikishindanishwa lakini bahati ndiyo hivyo haikuwa yake.

Akizungumzia namna alivyochukulia  kitendo cha Mobetto na Diamond kufika eneo hilo na kuweza kukabidhi tuzo, Wema ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Diamond miaka kadhaa iliyopita na hivi karibuni kuelezwa kwamba wamerudiana, amesema kitendo hicho kwake amekichukulia kawaida kwa kuwa Mobetto na Diamond ni mtu na mzazi mwenzake.

“Wee ulitaka nichukuliaje labda, Mobetto na Diamond hawa ni wazazi jamani , ulitaka nikasirike au,halafu isitoshe mimi sina uhusiano wa kimapenzi na Diamond  bali ni washkaji tu na siyo kama watu wanavyosema,”amesema Wema.

Kuhusu hatua yake ya kupata tuzo mbili ya msanii bora wa kike na chaguo la watu (People’s Choice Award) kupitia filamu yake ya ‘Heaven Sent’, Wema amesema amefurahi kuona majaji wameweza kuona kipaji alichonacho.

Pia, aliahidi kuendelea kuwapa mashabiki wake kazi nzuri na kuwaondoa hofu wadau wa filamu waliokuwa wanasema kuwa bongo movie imekufa kuwa siyo kweli bali ilikuwa imelala tu.

Hata hivyo, hakusita kutoa shukurani kwa mashabiki zake ambao amesema ni  kati ya watu ambao waliweza kushiriki kumpigia picha hadi kuhakikisha anapata ushindi huo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad