22 May 2018

Esha Ampa Makavu Jokate "Usinichukie Mimi wa Kumchukia ni Alikiba Mwenyewe Aliyeamua Kuoa"

Esha Ampa Makavu Jokate "Usinichukie Mimi wa Kumchukia ni Alikiba Mwenyewe Aliyeamua Kuoa"
ESHA Buheti amefunguka kuwa kama mwanamitindo maarufu Jokate Mwegelo, anamchukia kisa mwanamuziki Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’ kuoa, atakuwa anamkosea sana.

Akipiga stori na Over Ze Weekend, Esha ambaye amefanya poa kwenye filamu ya Jini Aulat, alisema kuwa ames-ikia kutoka kwa watu wake wa karibu kwamba mwanamitindo huyo anamchukia kwa sasa kutokana na kuwa karibu na Kiba kwenye harusi yake na mrembo Amina Khaleef wa Kenya.

Alisema mbali na hilo, pia anahisi hivyo maana tofauti na zamani Jokate alipokuwa akitazama vitu vyake mitandaoni na kumsapoti lakini siku hizi mrembo huyo hafanyi.“Kama ni kweli Jokate atakuwa ananichukia kisa mpenzi wake wa zamani Kiba kuoa kama watu wanavyosema, basi atakuwa ananichukia bure.

“Mimi ni kama bendera tu nafuata upepo kwa hiyo wa kumchukia ni Kiba mwenyewe aliyeamua kumuacha yeye na kuoa mtu mwingine, na wala si yeyote yule ambaye yupo karibu na Kiba,” alisema Esha.


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger