Waziri Majaliwa Amaliza Tatizo la Umeme Lindi na Mtwara

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri  Majaliwa Amaliza Tatizo la Umeme Lindi na Mtwara
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema shida ya umeme iliyokuwa inaikabili mikoa ya Lindi na Mtwara hivi sasa imekwisha.



“Kuunganishwa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara kwenye gridi ya Taifa, kumeondoa tatizo la umeme lililokuwa likiikabili mikoa hii, na mitambo ya jenerata iliyokuwepo, itabakia kuwa ya akiba endapo dharura yoyote itatokea,” alisema.



Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumatatu, Mei 21, 2018) wakati akizungumza na wakazi wa mji wa Mtwara kwenye viwanja vya bandarini mjini humo.



Alisema pengo lililokuwepo la kukatikakatika kwa umeme, limezibwa kwa kupata umeme wa kutoka Somanga hadi Lindi. “Umeme huu umeanzia kituo chetu cha Mbagala, umekuja Mkuranga, Muhoro, Lindi na hatimaye umefika pale Mahumbika. Na mchana wakati nikiwa Mahumbika, niliwasha kwa kompyuta kuashiria umeme wa gridi kuingia mikoa yetu ya Lindi na Mtwara,” alisema.



Akiwa Mtwara mjini, Waziri Mkuu alikagua na kisha kuzindua mradi wa upanuzi wa kituo cha kufua umeme wa gesi asilia wenye uwezo wa kuzalisha megawati nne.



Kabla ya kuzindua mradi huo, alipita bandarini kukagua ukarabati wa mitambo ya kupokelea mafuta ya dizeli na petroli ambako alielezwa kuwa kampuni mbili za GM na OILCOM zimeanza ukarabati na kwamba mwezi ujao, bandari hiyo itaanza kupokea meli za kubeba mafuta.



“Bandari ya Mtwara hivi sasa itaanza kupokea meli kubwa za mafuta, jambo ambalo halijafanyika tangu mwaka 2014. Mwezi ujao, wakati wowote, wataanza kupakua mafuta. Kwa hiyo mji utaanza kuchangamka.”



“Kuanza kupakuliwa kwa mafuta katika bandari hii, kutasaidia kushusha bei ya mafuta kwenye mikoa hii na pia kiasi kitakachobakia, tutakipeleka nchi za jirani za Msumbiji na Malawi,” alisema.



Alisema matengenezo hayo yakikamilika yatafanya bandari za Dar es Salaam, Mtwara na Tanga zote ziwe na uwezo wa kupokea mafuta. Pia aliitaka Mamlaka ya Bandari (TPA) iondoe urasimu na Mkurugenzi Mkuu wake awatumie vizuri watendaji waliopo chini yake.



Mapema, walipopewa nafasi ya kusalimia wananchi, wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF) walitumia fursa hiyo kuelezea kufurahishwa kwao na hatua za maendeleo zinazofanywa na Serikali ya awamu ya tano.



Zuberi Mohammed Kuchauka (Liwale) aliwataka wananchi wa mikoa ya Kusini wachangamkie fursa zinazopatikana kutokana na maendeleo yanayofanywa na Serikali ya awamu ya tano. “Kusini hivi sasa imeamka na imetoka gizani, sasa wananchi tuchangamkie fursa,” alisema.



Naye Mbunge wa Nachingwea, Bw. Hassan Elias Masala, alitumia fursa hiyo kuomba barabara ya kutoka Nachingwea iwekewe lami ili wakazi wake waweze kutumia fursa ya kusafirisha korosho zao hadi kwenye bandari ya Mtwara.



Naye Bw. Maftaha Abdallah Nachuma (Mtwara Mjini) pia aliomba barabara ya kutoka Mtwara hadi Mingoyo ikamilishwe matengenezo yake kwani kwa hali ya sasa siyo rahisi kusafirisha mizigo. Pia aliomba apelekewe umeme maeneo ya Mbawalachini na Mkunjanguo. “Maendeleo hayana chama, kabila wala itikadi,” alisema.



Wabunge wengine waliofuatana na Waziri Mkuu kwenye ziara hiyo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na Mbunge wa Mtwara Vijijini, Bibi Hawa Ghasia na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini, Bi. Hamida Mohammed Abdallah (Viti Maalum).
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad