Jeshi la Polisi Lamtia Mbaroni Aliyetumia Kisu Kumnyang'anya Bosi Wake Milioni 17

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Jeshi la Polisi Lamtia Mbaroni Aliyetumia Kisu  Kumnyang'anya Bosi Wake Milioni 17
Jeshi la Polisi Dodoma likiongozwa na Kamanda wake Gilles Muroto limemkamata Charles Mbise miaka 23 anayetuhumiwa kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha aina ya kisu ambapo anadaiwa kumpora mwajiri wake fedha zaidi ya Shilingi Million 17 katika kituo cha mafuta cha Afro Oil kilichopo Ipogolo mkoani Iringa na kisha kutaka kutorokea mkoani Arusha kwa kupitia Dodoma.

Muroto amesema…>>>”Mnamo July 16, 2018 huko Mkonze katika jiji la Dodoma katika kituo cha ukaguzi wa magari alikamatwa Charles Mbise mkazi wa Ipogolo Iringa ambaye. Mtuhumiwa alikamatwa kwenye gari namba T 165 DAD aina ya Costar wakati akijaribu kutoroka kwenda Arusha baada ya kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha aina ya kisu katika kituo cha Afro Oil kilichopo mkoani Iringa na kupora fedha za mwajiri wake kiasi cha Shilingi Milion 17”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad