Maelfu ya Wanawake na Watoto Waandamana Kumpinga Trump

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Maelfu ya Wanawake na Watoto Waandamana Kumpinga Trump
Maelfu ya watu wameandamana miji mbalimbali nchini Marekani kupinga msimamo wa Rais Donald Trump wa kukabili wahamiaji nchini humo.

Msimamo wa Trump ulisababisha watoto kutenganishwa na wazazi wao na kuwekwa katika mahema na vizuizi mbalimbali.

Trump alituma ujumbe kupitia mtandao wa kijamii akisema kuwa sheria za uhamiaji za nchi hii, (Marekani) ni za kijinga kuliko zote duniani” na kwamba wahamiaji warejeshwe katika nchi zao bila ya kupewa fursa ya kupitia mchakato wa kisheria kabla ya kuondolewa nchini.

Muungano wa wanaharakati, yakiwemo makundi ambayo yaliandaa maandamano makubwa ya wanawake miaka miwili iliyopita, wamesaidia kuratibu maandamano zaidi ya 600 katika miji mikubwa na midogo nchini humo.

Miji ambayo watu walijitokeza kuandamana ni pamoja na  Hawaii na Puerto Rico, kadhalika katika daraja la kimataifa kati ya El Paso, Texas na Juarez, Mexico na  Antler, North Dakota.

Mjini Washington, mtoto wa kike wa miaka 12 aitwaye Leah, ambaye wazazi wake ni wahamiaji wasio na kibali cha kuishi Marekani, alitoa ujumbe wenye hisia kali kwa watoto wote wahamiaji.

“Nataka niwaambie watoto walioko mpakani na nchi nzima wasikate tamaa na wapiganie kuungana na familia zao. Sisi sote ni binadamu na tunastahili kupendwa na kusimamiwa! Sisi ni watoto!” aliuambia umati mkubwa uliokuwa ukimshangilia.

Mchungaji wa ngazi ya juu wa kanisa la The King United Church of Christ, Missouri, Traci Blackmon, aliuambia umati wa waandamanaji mjini Washington, “Tulikuwa katika njia hii siku za nyuma. Lazima tusisahau hili. Lazima tukumbuke siku zote hili si tu suala la sera salama ya uhamiaji bali ni itikadi ya ubinafsi.”

Kadhalika mjini Washington, Lin-Manuel Miranda, aliyebuni muziki wa “Hamilton” aliimba wimbo uliokuwa mahsusi kuwaliwaza wazazi ambao hawana uwezo wa kuwaimbia watoto wao ambao wamechukuliwa kwa nguvu kutoka mikononi mwao.

Waandamanaji huko New York, ambako ni nyumbani kwa Trump, walikuwa wakiimba “Hakuna chuki, hakuna vitisho, wahamiaji wanakaribishwa hapa Marekani!” huku kukiwa na jua kali walivuka daraja la Brooklyn kwenda katika moja ya uwanja wa kitongoji cha Brooklyn.

Wakati wakiandamana kuvuka daraja, wengi wao waliimba “Ni aibu.” Madereva wa magari walipiga honi kuunga mkono maandamano hayo.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Top Post Ad