TCRA Yazindua Rasimu ya Kkataba kwa Wateja

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

TCRA yazindua rasimu ya mkataba kwa wateja
Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA imezindua rasimu ya mkataba kwa wateja sambamba na kampeni ya kupambana na rushwa ndani ya mamlaka hiyo.

Lengo la rasimu hiyo ni kuweka ufanisi na uwazi katika kazi za mamlaka hiyo.

Akizungumza leo Jumatatu Julai 16, 2018 Mkurugenzi wa TCRA, mhandisi James Kilaba amesema mkataba huo utabainisha viwango vya utoaji huduma kwa wateja na haki na wajibu wa wateja kulingana na huduma zinazotolewa.

Amesema TCRA itatumia mkataba huo kama nyenzo muhimu ya kuzuia na kupambana na rushwa  kama inavyopewa uzito na Rais John Magufuli.

“Ndani ya mkataba huu tutawaonyesha wateja huduma tunazotoa, viwango vya hudumana uhusiano kati ya watumishi na wateja. Mkataba huu pia unalenga kuongeza tija na uwajibikaji kwa watumishi wa TCRA katika kutoa huduma bora kwa wateja wetu,"amesema.

Amebainisha kuwa hatua hiyo itawezesha dhamira ya ukweli na uwazi katika kazi zao kutimia, kubainisha kuwa kutimia kwa dhamira hiyo  itakuwa kinga ya kuzuia malalamiko ambayo yanaweza kutafsiriwa na wananchi kuwa ni vitendo vya rushwa.

“Upatikanaji wa habari sahihi bila vikwazo utaongeza uwazi na uwajibikaji wa kila mtumishi na hivyo itapunguza malalamiko,” amesema na kwamba mkataba huo utaendelea kuboreshwa kulingana na mahitaji ya utoaji huduma.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad