Whatsapp Yawaponza Shule ya Jangwani Hadi Kushika Mkia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

 Whatsapp Yawaponza Shule ya Jangwani  Hadi Kushika Mkia
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi, Selemani Jafo amefunguka na kudai chanzo kikubwa kilichopelekea shule ya sekondari Jangwani kushika mkia kwenye matokeo ya kidato cha sita ni kutokana na wanafunzi hao kujihusisha na uhasherati pamoja na matumizi ya Whatsapp.


Mrembo Jokate akiwa na baadhi ya wanafunzi wa Jangwani katika project zake za Netball. Picha hii sio ya tukio la hivi karibuni

Waziri Jafo ametoa kauli hiyo leo Julai 17, 2018 wakati alipokuwa shuleni hapo na kumuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam kufanya mabadiliko katika safu ya uongozi wa shule hiyo kwa kuwa hajaridhishwa na ufaulu wa wanafunzi kwa sababu Jangwani ndio shule ya ndoto ya wasichana wengi wa kitanzania.

“Shule ya Jangwani ni shule ambayo yenye upako maalum, sifa na tunu kwa nchi yetu lakini shule hii sasa imekuwa ya tatu kutoka mwisho. Hii ni fedheha ambayo haijawahi kutokea katika shule ya Jangwani. Wanafunzi mmekuja hapa kwaajili ya kusoma sio kwa sketi zenu za rangi ya chungwa, tunataka msome…..

Kwa taarifa nilizozipata wanafunzi wanatumia simu hizi za Whatsapp na muda mwingi wanaangalia picha zilizokuwa mbovu badala ya kusoma huku wengine wakikalia ku-chat na kuangalia vitu ambavyo sio sawa sawa”, amesema Jafo.

Pamoja na hayo, Jafo ameendelea kwa kusema “kwa taarifa nilizozipata hapa za kiuchunguzi ni kwamba wanafunzi wengi wanajihusisha na mambo ya uhasharati, naomba niwaambie endapo mtajihusisha na mambo hayo, elimu haitaweza kuwa rafiki yenu na hilo jambo hata wakubwa wazima linawashughulisha sembuse nyie wanafunzi, nasema kuanzia leo hilo suala lishindwe na ndio maana ufaulu wenu unakuwa mbovu”.

Shule hiyo kongwe iliyopo eneo la Jangwani Jijini Dar es Salaam imeingia kwenye nafasi ya 10 shule zilizoweza kufanya vibaya katika matokeo yaliyotangazwa Julai 13, 2018 na Baraza la Mitihani la Tanzania (Necta).

Shule 10 za mwisho kitaifa ni Jangwani ya mkoani Dar es Salaam, Jang’ombe (Mjini Magharibi), Forest Hill (Morogoro), St James Kilolo (Iringa), Aggrey (Mbeya), Nyailigamba (Kagera), White Lake (Dar es Salaam), Musoma Utalii (Mara), Golden Ridge (Geita) na Ben Bella (Mjini Magharibi).

Huku shule 10 zilizoweza kufanya vizuri zaidi zikiwa ni Kibaha ya Mkoani Pwani, Kisimiri (Arusha), Kemebos (Kagera), Mzumbe (Morogoro), Feza Boys’ (Dar es Salaam), Marian Boys (Pwani), Ahmes (Pwani), St, Mary’s Mazinde Juu (Tanga), Marian Girls (Pwani) pamoja na Feza Girls ya Dar es Salaam.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwanini wanafunzi wanaruhusiwa kuingia na simu darasani? Ikwezekana waziache nyumbani kabisa. Au ni kupata msaada wa kitaaluma kutoka kwa wenzetu wa serikali ya china jinsi ya kuzibiti mtandao wa simu za wanafunzi katika eneo la shule ni kitu rahisi sana.

    ReplyDelete

Top Post Ad