Dk Bashiru: Hadi Sasa CCM Imetekeleza Nusu ya Ahadi Zake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Dk Bashiru: Hadi Sasa CCM Imetekeleza Nusu ya Ahadi Zake
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ali amesema tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani, imefanikiwa kutekeleza nusu ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015/20.

Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Agosti 13, 2018 jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kumtambulisha aliyekuwa mbunge wa Liwale (CUF), Zuberi Kuchauka, ambaye leo amejiunga na CCM.

“Chama chetu kimeendelea kujisahihisha pale yanapotokea makosa, lengo kuu ni kuhakikisha misingi ya Azimio la Arusha na Mapinduzi ya Zanzibar yanaimarishwa,” amesema.



“Katika kipindi hiki chini ya Rais John Magufuli tuko nusu ya utekelezaji wa Ilani yetu na bado tuna nusu nyingine, na katika ilani hiyo tunazo shabaha kubwa nne.”



Amezitaja shahaba hizo kuwa ni kupambana na umaskini wa wanyonge, kutengeneza nafasi nyingi za ajira hususani katika sekta ya kilimo, uvuvi, mifugo na viwanda, kupambana na rushwa na ufisadi na kuimarisha vyombo vya ulinzi na usalama ili Taifa liendelee kuwa na amani.

Amesema maeneo hayo yanatumiwa na wananchi kuwapima, kuwahoji na kuwaunga mkono. 

Amesema kazi inayoendelea kufanywa na Serikali kwa kusogeza zaidi huduma kwa wanyonge na wavuja jasho,  imesaidia kurejesha imani ya wananchi kwa chama hicho, kutolea mfano ushindi uliopata CCM katika uchaguzi mdogo wa ubunge na madiwani uliofanyika jana.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad