Mambo Yote Sauzi Leo Daimond na Zari Ndani ya Kitanda Kimoja

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mambo Yote Sauzi Leo Daimond na Zari Ndani ya Kitanda Kimoja
Kama ulikuwa unajiuliza kwamba itakuwaje siku ‘watalaka’, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ watakapokutana kwenye bethidei ya mtoto wao wa kike, Latiffah Nasibu ‘Tiffah Dangote’ kwamba watalala chumba kimoja au nyumba tofauti, ondoa shaka, jibu limepatikana.Ijumaa limehakikishiwa kuwa, mastaa hao watalala chumba kimoja. Bethidei ya Tiffah iliyozua gumzo kwenye mitandao ya kijamii kwa takriban mwezi mzima, inatarajia kuanza kuunguruma leo pande za Afrika Kusini ‘Sauz’ na kufikia kikomo siku ya Jumatatu, Agosti 20, mwaka huu.

TAARIFA ZA UHAKIKA

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ndani ya familia, Diamond ambaye hadhira inamtazama kuwa haziivi na mzazi mwenzake, Zari, nyuma ya ‘kamera’ zinaiva kwani wanawasiliana mara kwa mara na kwamba suala la yeye kwenda na kulala Sauz si jipya tangu wagombane.

“Wewe unafikiri kwamba Diamond na Zari ndiyo hawawezi hata kulala chumba kimoja kwa sababu tu wameachana? Siyo kweli, wale wanaweza kabisa kulala bila wasiwasi na hata kwenye hii bethidei watakapokutana, watalala chumba kimoja bila tatizo,” kilimwaga ubuyu chanzo cha kuaminika.

Chanzo hicho kilikwenda mbele zaidi kwa kueleza kuwa, hivi karibuni, Diamond aliekwenda Sauz na akalala baada ya kutoka kwenye shoo zake nchini Marekani. “Wewe hukuona picha zile Diamond alipiga yupo kitandani na wanaye na aliziposti hata kwenye akaunti yake ya Instagram? Sasa kwa taarifa yenu alikwenda na akalala chumba kimoja na Zari,” kilidai chanzo hicho.

WAMEMALIZA TOFAUTI?

Chanzo h icho kilipoulizwa endapo wawili hao wameshamaliza tofauti zao na kwamba wanaendeleza uhusiano wao kwa usiri mkubwa hakikukubali wala kukataa.

“Mh! Kwa kweli hapo sasa mimi nitaongea nini? Sioni kama ninaweza kuwa na jibu la moja kwa moja, ninachoweza kukuhakikishia tu ni kwamba ishu ya Zari kulala na Diamond ni jambo la kawaida,” kilisema chanzo hicho.

MAMA D FULL VICHEKO

Chanzo hicho kiliongeza kuwa, mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye ameonekana kuwa upande wa Zari kuliko mwanamke mwingine yeyote aliyezaa na mwanaye, ana furaha isiyoelezeka. “Mama Dangote (mama Diamond) furaha imeongezeka maradufu maana Zari ndiye kipenzi chake na ukizingatia Tiffah ni mjukuu wake kipenzi,” alisema mtu wa karibu wa mama D.

MAANDALIZI KUSUASUA

Kutokana na kuwepo kwa kusuasua kwa shamrashamra kama ilivyokuwa awali kuhusu bethidei ya Tiffah, Ijumaa lilimchimba zaidi sosi huyo ambaye pia ni mwanafamilia ili kujua kama kweli sherehe ipo au haipo.

Ijumaa: Awali tuliona promo ilikuwa kubwa sana mitandaoni, kamati ya 40 ya mtangazaji Zamaradi Mketema ilipewa ofa ya kwenda kisha zengwe likaingia kwamba Zari amewazuia wasiende, watachafua nyumba, vipi safari ya Sauz ipo au haipo?

Chanzo: Ipo palepale, watu wataenda kama ilivyopangwa.

Ijumaa: Mbona zile promo zimepungua sana? Hatujui hata wale watoto 10 waliopewa ofa ya kwenda pamoja na wazazi wataenda?

Chanzo: Wewe subiri siku ya safari kati ya Alhamisi (jana) au Ijumaa (leo), utatuona ndani ya ndege.

DIAMOND ANASEMAJE?

Ijumaa lilimbananisha Diamond mapema wiki hii ili aweze kuzungumzia ishu hiyo, lakini alipopatikana hakutaka kuzungumza kitu kiginine tofauti na maudhui ya ‘presi’ yake aliyokuwa ameiandaa.

TALE ATHIBITISHA

Ijumaa lilizungumza na meneja wa Diamond, Hamis Taletale ‘Babu Tale’ ambaye alithitisha kuwa safari ya Sauz kwa watu wote waliowatajwa iko palepale. “Unajua hii ni pati, bethidei ya Tiffah ilishapita, lakini nikwambie tu, itafanyika na kutakuwa na sapraizi mtaona,” alisema Tale.

Alipoulizwa zaidi kuhusu wanakamati wa sherehe ya 40 ya mtangazajia Zamaradi ambao walipewa ofa na Diamond kwenda kwenye pati hiyo kisha kuibuka kwa utata kufuatia kauli ya Zari, Tale alisema kamati hiyo itaenda licha ya kuwa kuna vitu wanaviweka sawa.

“Kuna vitu vinawekwa sawa lakini pia kuna suala la pasipoti, wengine hawana kwa hiyo inakuwa ni changamoto yao,” alisema Tale. Alipobanwa maswali zaidi juu ya namna itakavyokuwa siku ya bethidei na kama Zari na Diamond watalala chumba kimoja, Tale hakuwa tayari kufafanua kwa undani.

MAMA DIAMOND ANENA

Ijumaa lilimtafuta mama Diamond na kumuuliza juu ya maandalizi ya safari hiyo na endapo wataitumia pia kumaliza tofauti za mwanaye na Zari, lakini alipopatikana hakutaka kuzungumzia suala hilo licha ya kukiri kuwa safari yao ipo kama kawaida.

“Wewe ukitaka kuniuliza kuhusu safari nitakujibu tu ipo palepale, lakini hayo mambo yenu mengine ya kidaku mimi siwezi kuyajibu,” alisema mama Diamond.

TAARIFA ZA KUSOGEZWA MBELE

Wakati Ijumaa lilipokuwa linakwenda mitamboni, ilielezwa kuwa Zari alipata msiba wa ndugu wa aliyekuwa mume wake, marehemu Ivan Ssemwanga hivyo sherehe hiyo kuwa na ‘hatihati’ ya kusogezwa mbele hadi baadaye, mwishoni mwa mwezi huu.

TUJIKUMBUSHE

Kwa kawaida, bethidei ya Tiffah huadhimishwa Agosti 6 kila mwaka, lakini kwa mwaka huu Diamond alishindwa kujumuika pamoja na mwanaye kutokana na shughuli za kimuziki hivyo kulazimika kumuandalia sherehe aliyopanga kuifanya Agosti 17, mwaka huu huko Sau
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad