Polepole Afunguka Ishu ya Rais Kuteua Viongozi Kutoka Upinzani “CCM haitazami historia ya mtu”

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Polepole Afunguka Ishu ya  Rais Kuteua Viongozi  Kutoka Upinzani  “CCM haitazami historia ya mtu”
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amefunguka kuhusiana na Mwenyekiti wake, Dkt. John Magufuli kuwateua viongozi wanachama wapya waliotoka upinzani, ambapo amedai kuwa CCM haitazami historia ya mtu.

Polepole amesema hayo katika mahojiano maalum na www.eatv.tv ,ambapo amefunguka kuwa, si kila mwanachama wa CCM anasifa za kuwa kiongozi kwani kazi ya chama ni kuandaa raia wema na wanachama waaminifu.

“Chama cha Mapinduzi kina zaidi ya wanachama milioni 12-14, hivyo basi kwa wingi huo haiwezekani wote tukaingia kwenye chama tukiwa na fikra ya uongozi, cheo ni dhamana na kila mwana CCM ana haki sawa za kupata nafasi ya uongozi, ukishakuwa kuwa mwanachama wetu hatutazami historia tunachotazama ni vigezo vya uongozi”, amesema Polepole.

Hayo yamejiri baada ya Rais Dkt. Magufuli, Julai 28, 2018  kufanya mabadiliko ya wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu tawala, makatibu wakuu na manaibu wao,  huku akiteua wanasiasa waliotokea vyama vya upinzani.

Walioteuliwa ni pamoja David Kafulila aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali (Kasulu Mjini, NCCR Mageuzi), na Patrobas Katambi (aliyekuwa mwenyekiti Baraza la Vijana la Chadema, wote wakiwa wamejiunga na CCM kati ya mwaka jana na mwaka huu.

Katambi amekuwa mkuu wa wilaya ya Dodoma, wakati Machali anaenda Nanyumbu na Kafulila ambaye anakuwa katibu tawala wa mkoa Songwe.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad