Waziri Lugola Amuweka Ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Lugola Amuweka Ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi
Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Kangi Lugola amemweka ndani Mkuu wa Kituo cha Polisi Mtwara mjini, Ibrahim Mhando kwa kosa la kuweka watuhumiwa chumba cha upelelezi badala ya mahabusu kituoni hapo.


Waziri Kangi Lugola amefikia hatua hiyo baada ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo (RPC), Mkondya kumweleza Waziri Lugola kituoni hapo kuwa, Polisi wake walifanya makosa kwa kutowaweka watuhumiwa hao mahabusu.

''Tabia hii siku zote tunaipinga imekuwa ikichafua Jeshi la Polisi, na hii ndiyo tabia yenu, najua ndio maana nimekuja ghafla, OCS umeweka hawa watuhumiwa chumba cha upepelezi badala ya mahabusu, sasa na wewe unaingia ndani'', amesema Kangi wakati akimweka ndani OCS Ibrahim Mhando.

Mkuu huyo wa Kituo cha Polisi cha Kati mjini Mtwara (OCS), Ibrahim Mhando, alishindwa kuwaweka mahabusu watuhumiwa wanne akiwemo Mhandisi Mshauri wa Kampuni ya Y&P Architects.

Mbali na hilo Waziri Kangi pia amemhoji Mkurugenzi wa Ufundi wa Kampuni ya Ujenzi ya Lucas Theophilius Kessy, ambaye ndiye kandarasi aliyejenga Jengo la Uhamiaji Mkoa wa Mtwara chini ya kiwango.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad