Dawasco Yavunjwa Rasmi ......Yaunganishwa Na Dawasa...Sababu Kubwa Hizi Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Shirika la majisafi na Majitaka Dar es Salaam(DAWASCO) limevunjwa rasmi na kuunganishwa katika Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(DAWASA).

Akizungumza katika sherehe za kuunganishwa kwa DAWASA na DASAWCO leo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Profesa Kitila Mkumbo amesema kuunganishwa huko kutaokoa Sh Bilioni 2.9 kila mwaka zilizokuwa zikipotea katika uendeshaji wa Dawasa na Dawasco.

Amesema fedha hizo zitakwenda kusaidia upatikanaji wa huduma ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani.

“Serikali iliamua kuunganisha Dawasa na Dawasco ili kupunguza matumizi na fedha hizi zitaimarisha miundombinu na kuboresha huduma za maji katika eneo la huduma,” alisema Profesa Mkumbo.

Profesa Mkumbo amewaonya wafanyakazi wa Dawasa mpya kuacha tabia ya ya dharau, nyodo,kukumbatia matatizo, na kuomba rushwa kwa wateja.

“Baadhi yenu mmekuwa na nyodo, kikola,rushwa na kuridhika na mafanikio kidogo tabia hizi zikome kuanzia sasa,” alisema Profesa Mkumbo.

Ametaka Dawasa mpya kujiendesha kama kampuni binafsi inayolipwa na wananchi wa Dar es Salaam na si Idara ya serikali ili kuongeza makusanyo ya fedha.

“Niwaombe mpunguze upotevu wa maji ambao kwa sasa asilimia 47 ya maji yanayozalishwa na Dawasa yanapotea,” alisema Profesa Mkumbo.

Aidha alisema serikali imeamua kuwapa Dawasa jengo la ghorofa lililopo Ubungo njiapanda ya kwenda chuo kikuu ili walimalizie na kuhamia humo.

Kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa, Cyprian Luhemeja ameahidi kuteteleza baakukamilisha miradi mitatu na kutoa muendelezo wa miradi mingine ndani ya siku 100.

“Zawadi yetu kwa Rais Dk John Magufuli hadi kufikia Disemba 9, mwaka huu tutakamilisha mradi wa maji wa Chalinze, usambazaji wa maji upande wa Goba tegeta na maeneo mengine yaliyokaribu,” alisema Luhemeja.

Amesema  ndani ya siku 100 hizo watafunga mita za malipo ya kabla nyingi na kuwahakikishia wanaanza ujenzi wa matenki ya Pugu na kusanifu upya mradi wa visima vya Mpera.

“Ndani ya siku hizo pia tutaongeza mapato kutoka Sh Bilioni tisa hadi kufikia Sh Bilioni 12 na pia tutahakikisha tunapunguza upotevu wa maji,” alisema Luhemeja
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad