Makamu wa Rais Kuzindua Jengo la Kitega Uchumi la Ghorofa 16 Jijini Arusha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makamu wa Rais Kuzindua Jengo la Kitega Uchumi la Ghorofa 16 Jijini Arusha
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwaongoza maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Arusha katika hafla ya uzinduzi wa jengo la kitega uchumi la Jakaya Kikwete Ngorongoro Tower (JKNT).

Jengo hilo la ghorofa 16, ambalo ni mali ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), linatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais, Septemba 16, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati walipotembelewa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Arusha, kukagua jengo hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya NCAA, Profesa Abiud Kaswamila, alisema Makamu wa Rais amethibitisha kuhudhuria katika hafla ya uzinduzi wa jengo hilo.

Alisema jengo hilo ni kati ya majengo ya kisasa zaidi kujengwa mkoani hapa na litatumika maalum kama kituo kimoja cha kukuza na kurahisisha biashara ya utalii nchini.

Maneja wa mradi wa ujenzi wa jengo hilo, Profesa Camillius Lekule, ambaye ndiye aliyebuni mchoro wa jengo hilo, alisema kiasi cha fedha zilizotumika hadi sasa ni Sh. bilioni 39.9 kati ya Sh. bilioni 45 zilizokadiriwa awali.

Alisema matarajio ya NCAA baada ya kuwekeza fedha nyingi katika ujenzi wa mradi huo gharama za ujenzi zitarudi baada ya miaka 20.

Alisema jengo hilo lina uwezo wa kudumu kwa miaka 100 ijayo bila ya kupoteza ubora wake na uhalisia kutokana na ujenzi wa kitaalam uliotumia vifaaa vya kisasa na vyenye ubora zaidi.

Lekule alisema usanifu wa jengo hilo ulianza Januari 2011 na ujenzi ulianza Novemba 7, mwaka 2013 na sasa upo katika hatua za mwisho kukamilika.

Naye Meneja Uwekezaji wa NCAA, Needpeace Wambuge, alisema jengo hilo ni maalum kwa ajili ya kitega uchumi cha biashara ya utalii ili kuendeleza utalii baada ya kutokea kwa mtikisiko kwenye sekta hiyo, ulioathiri shughuli za utalii sehemu mbalimbali nchini.

Aidha alisema hadi sasa asilimia 45 ya jengo hilo limeshapangishwa na wadau mbalimbali na gharama za ukusanyaji wa mapato kwa mwezi zitafikia kiasi cha Sh. milioni 350, na kwa mwaka mzima kodi inayotarajiwa kukusanywa ni Sh. bilioni 4.3.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad