Mechi ya Ndanda FC dhidi ya Simba Kutimua Vumbi Nangwanda Sijaona Leo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mechi ya Ndanda FC dhidi ya Simba Kutimua Vumbi Nangwanda Sijaona Leo
Yakiwa yanasubiriwa masaa masaa tu kuelekea pambano la mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Ndanda FC dhidi ya Simba, kuna uwezekano mkubwa timu hiyo ikawakosa nyota wake muhimu.

Simba itakutana na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona kuwania alama tatu muhimu ili kujitengenezea mazingira ya kuutetea ubingwa wake baada ya kuubeba msimu uliopita.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu, Patrick Aussems, amesema kuwa kiungo Mzambia, Clatous Chama, hatoweza kumtumia baada ya kuchelewa kuripoti kambini.

Mbali na Chama, wachezaji wengine Mnyarwanda, Haruna Niyonzima pamoja na Mganda Juuko Murushid nao wanaweza wakaukosa mchezo huo baada ya kukosekana mazoezini kwa muda mrefu.

Niyonzima alichelewa kuripoti kambini na hata katika safari ya Uturuki hakuwepo sawa na Murushid ambaye alikuwa kwenye sintofahamu na mabosi wake alikuwa kwao Uganda.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad