Serikali yasema michango ya ajali MV Nyerere iko sehemu salama

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Serikali imesema fedha zote zilizochangwa kwa ajili ya ajali ya kuzama kwa Kivuko cha MV Nyerere, zimehifadhiwa sehemu salama.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, amesema hayo leo katika Kijiji cha Bwisya, wilayani Ukerewe akitoa salamu katika mazishi ya halaiki.


Amesema fedha hizo zilizochangwa na Watanzania na wasio Watanzania zinahifadhiwa sehemu salama kwa shughuli husika na tayari imefunguliwa akaunti kwa ajili hiyo.


“Pia tutafungua akaunti ya Tigopesa ili watu waendelee kuchangia na kama nilivyosema awali zitafanya shughuli husika,” amesema Jenista.


Pamoja na mambo mengine, amesema pamoja juhudi zilizofanywa na wananchi na watu mbalimbali serikali imefanya kazi kubwa ikiwamo kutoa mchango mkubwa wa vifaa tiba kwa walionusurika na kuhifadhi waliofariki.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad