Waziri Lukuvi azipiga marufuku kampuni binafsi katika upimaji ardhi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Waziri Lukuvi azipiga marufuku kampuni binafsi katika upimaji ardhi
Serikali kupitia kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi imepiga marufuku kampuni binafisi za upimaji ardhi ambazo zimekuwa zikiingia makubaliano ya upimaji ardhi za wananachi bila hata uongozi wa Wilaya husika kuwa na taarifa.


Lukuvi amesema kuwa kuanzia sasa nchini kote hakuna Kampuni binafsi ya aina yoyote inaruhusiwa kwenda na kuingia moja kwa moja makubaliano na wananchi ya kuwapimia maeneo yao bila hata kutoa taarifa kwa uongozi wa Wilaya husika.

Hayo yamejiri kufuatia wakazi wa baadhi ya maeneo ya Manispaa ya Tabora kuilalamikia Kampuni ya Ardhi Plan kuwachangisha fedha zao bila ya kupimia ardhi yao.

Aidha, amesema haiwezekani upimaji wa ardhi za wanyonge ukageuza uchochoro wa kuwaibia na kuwadhulumu wananachi haki zao na kuongeza kuwa lazima sheria na taratibu zifuatwe katika upimaji wa ardhi za wananchi na taarifa ziwe kwa Wakuu wa Wilaya.

Huku Waziri Lukuvi akiongeza kuwa Kampuni za aina hiyo zimekuwa zikiwachangisha fedha na kugawana mapato bila hata ya kuwapimia wananchi huku uongozi wa Wilaya husika ukiwa hauna hata taarifa. Na kuzitaka halmashauri zote za Mkoa wa Tabora kutumia Chuo cha Ardhi Tabora na kuachana na Kampuni za nje kupima ardhi ili kuepuka matumizi makubwa ya gharama za zoezi hilo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad