Waziri Majaliwa Agusa Dawa za Kulevya China

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Majaliwa agusa dawa za kulevya China
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Watanzania waishio nje ya nchi wajiepushe na vitendo vya uhalifu hasa biashara ya dawa za kulevya  ambayo inachafua jina na heshima ya nchi kimataifa.


Majaliwa ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo Septemba 3, 2018, kwenye ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini China uliopo jijini Beijing  wakati akizungumza na Watanzania waishio humo.

“Nawasihi wote mnaoishi nje muachane kabisa na biashara haramu ya dawa za kulevya kwa sababu inalitia doa Taifa na adhabu yake katika baadhi ya nchi ni kifo pia tukumbuke Tanzania ni nchi nzuri na inaheshimika duniani kwahiyo tuilinde heshima hiyo,” alisema.

Mbali na hilo Majaliwa pia amewataka Watanzania waishio nje ya nchi  wahakikishe wanashiriki kikamilifu kujenga uchumi wa nchi yao  kwa kushawishi wawekezaji wenye mitaji mikubwa waje kuwekeza nchini na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania.

Miaka ya hivi karibuni imekuwa ikiripotiwa biashara ya dawa za kulevya kuhusisha watanzania ambao mara nyingi huwa wanakumbana na adhabu za mataifa hayo ikiwemo kufungwa maisha, kunyongwa na muda mwingne kifo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad