Ajali Mbaya ya Gari Yaua Watano Singida

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ajali Mbaya ya Gari Yaua Watano Singida
Watu watano wameripotiwa kupoteza maisha kwenye ajali ya gari iliyotokea eneo la Njirii wilayani Manyoni mkoani Singida leo Oktoba 21.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, kamshina msaidizi wa polisi Sweetbert Njewike, amesema kuwa ajali hiyo imehusisha magari mawili ikiwemo gari dogo mali ya Wizara ya Kilimo na Chakula iliyokuwa na watu watano pamoja na lori.

Kamanda Njewile amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari ndogo iliyokuwa katika mwendokasi ikijaribu kupishana na lori.

"Gari ndogo mali ya Wizara ya Kilimo na Chakula ilikuwa ikitokea Dodoma kwenda Shinyanga ikiwa na watumishi wa wizara hiyo, ilikuwa katika mwendokasi na kugongana uso uso na Lori", amesema Kamanda Njewile.

Kamanda amewataja waliofariki kuwa ni wanawake wawili na wanaume watatu na wote wamehifadhiwa katika hospitali ya Wilaya ya Manyoni.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad