Baada ya January Makamba Kuhojiwa na Polisi Kuhusu Mo Dewji Afunguka Haya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Baada ya January Makamba Kuhojiwa na Polisi Kuhusu Mo Dewji  Afunguka Haya
Mapema leo asubuhi kulichipuka taarifa za kuwa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemhoji kwa saa kadhaa na kumwachia Waziri January Makamba kuhusiana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara Mohammed Dewji.

Januaary Makamba ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano ameeleza kile alichoitiwa na Polisi. Kupitia ukurasa wake wa Twitter waziri huyo ameandika; ,

Ufafanuzi: Polisi walinipigia simu kuniomba, kama rafiki wa MO Dewji, niwasaidie kama kuna chochote cha ziada ambacho Mo aliniambia kinachoweza kusaidia uchunguzi. Niliwaeleza. Wakasema kinafanana na alichowaeleza. Wakanishukuru. Wamefanya hivi pia kwa wanafamilia. Sikukamatwa.

Utakumbuka alfajiri ya October 19, 2018 January Makamba ni miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kueleza kuwa Mfanyabiashara maarufu Tanzania Mohammed Dewji amerejea nyumbani akiwa salama baada ya kushikiliwa na watekaji kwa takribani siku 10.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad