13 Oct 2018

Babu Tale na Hawa wa Diamond Wazuiliwa Kusafiri Kwenda India Jioni Hii..Chanzo Hiki Hapa


BABU TALE NA HAWA WA DIAMOND WAZUILIWA KUSAFIRI KWENDA INDIA JIONI HII, CHANZO HIKI HAPA |

Msanii Hawa Said maarufu Hawa wa Diamond, amejikuta akirudishwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA) baada ya kutotimiza vibali vya kusafiri vya kimatibabu kwenda India.

Akizungumza na MCL Digital baada ya kukwama leo Oktoba 13, 2018  meneja wa Diamond Platinumz ambao ndiyo wamechukua jukumu la kugharamia matibabu hayo, Babu Tale amesema hali hiyo imewakuta wakiwa tayari wameingia ndani ya uwanja wa ndege na kuanza kukaguliwa nyaraka zao mbalimbali.

Babu Tale amesema nyaraka iliyowakwamisha kusafiri ni kibali cha daktari kuelezea hali ya mgonjwa  ili wahudumu ndani ya ndege wajue namna watakavyomhudumia. "Kuna mgonjwa anaweza akawa katika hali ya kuzimia, kutapika anatakiwa ahudumiwe tofauti, hivyo Hawa imeshindikana kwa kuwa hakuna hizo nyaraka inayoonyesha hivyo kutoka kwa daktari na wametwambia turudi itakapokamilika," amesema.

Hawa, Babu Tale na mama yake, Ndagina Hassan ilikuwa waondoke leo  saa 10:45 na ndege ya Shirika la Emirates.

Hawa na mama yake, Ndagina, walifika uwanjani hapo tangu saa 7:00 mchana huku Babu Tale akiwasili saa 9:00 alasiri.

MCL Digital iliyokuwa imepiga kambi wakati wote uwanjani hapo, ilifanikiwa kuzungumza na mama wa Hawa ambaye ameelezea furaha yake ya mwanaye kupata msaada wa matibabu.

Naye Hawa amewaomba Watanzania kumuombea dua katika matibabu hayo.

Awali, Babu Tale amesema walitarajia kuwa nchini humo kwa wiki mbili na huenda Hawa akapandikizwa ini kama madaktari watashauri hivyo.

Mwananchi


Install Application ya Udaku Special Uweze Pata Habari Kama Hizi Kirahisi Zaidi
=>BOFYA HAPA KUINSTALL/DOWNLOAD
Weka Maoni yako Hapa

0 facebook:

Post a Comment

Nafasi za Kazi

Popular Posts

Copyright © UDAKU SPECIAL BLOG | Powered by Blogger