CCM walitupora jimbo la Liwale - CUF

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

CCM walitupora jimbo la Liwale - CUF
Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), anayetambulika na msajili wa vyama vya siasa nchini, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Kaliua, Magdalena Sakaya amesema kuwa suala la chama hicho kuendelea na chaguzi za marudio zinazondelea litajadiliwa na litatolewa maamuzi hivi karibuni.

Sakaya amesema kuwa kikao hicho kitatoa majibu endapo wataendelea au watajiondoa kwa yale yanayojitokeza kwenye chaguzi zilizopita ikiwemo mawakala wake kutopewa fomu za kusimamia kura katika baadhi ya vituo.

Sakaya amefunguka hayo katika mahojiano na www.eatv.tv, ambapo amesema kuwa uchaguzi uliopita katika jimbo la Liwale CUF walionewa na kuporwa jimbo hilo ambalo lilikuwa ni ngome yao.

"Nilikuwepo Liwale nmeshuhudia kila kitu, CCM wametuibia kura zetu kwani asilimia 75 ya wapiga kura waliipigia kura CUF lakini mawakala wetu walinyimwa fursa ya kusimamia na kuhesabu kura zetu", amesema Sakaya.

Marudio ya uchaguzi wa jimbo la Liwale yalifanyika, Oktoba 13, baada ya aliyekuwa mbunge wake Zuberi Kachauka (CUF) kujiuzulu na kujivua uanachama na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM), ambapo aliteuliwa kuwa mgombea kupitia chama hicho na baadae kuibuka mshindi katika uchaguzi huo wa marudio.

CHADEMA kupitia mwenyekiti wake wa chama, Freeman Mbowe kilitangaza kujiondoa rasmi kushiriki chaguzi ndogo zote zilizotangazwa kufanyika hivi karibuni na chaguzi zozote zitakazofuata zinazosimamiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa madai kwamba tume hiyo inafanya kazi kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad