Monalisa Adaiwa Kumwaga Machozi Ukumbini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Ivyonne Cherry maarufu kama Monalisa amedaiwa kuangua kilio ukumbini baada ya kuguswa na mabinti wanatarajia changamoto Kwenye sanaa.

Monalisa alishindwa kujizuia pale alipokuwa anawaongelea jinsi wasichana wadogo wanavyonyanyaswa kingono sehemu wanazokwenda kuomba kusaidiwa ili kuingia katika sanaa.

Monalisa aliangua kilio hicho ndani ya Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo alikuwa akizindua mpango wa kuwaendeleza mabinti wenye vipaji vya kuigiza uitwao Monalisa ACT.

Mona alifunguka kuwa anajua mabinti wengi wakienda kwa watu kuomba kusaidiwa ili waoneshe vipaji vyao, wengi huishia kudhalilishwa kingono ndipo wasaidiwe, jambo ambalo alililaani vikali.

Ukweli mabinti wengi wana vipaji vya filamu lakini wanaishia kukata tamaa na vipaji vyao kupotea, hii ni kwa sababu wanapokwenda kuomba msaada wameishia kuombwa rushwa ya ngono, jambo ambalo siyo zuri kabisa“.

Alifunguka Mona huku machozi yakimlengalenga na hata aliposhuka na kwenda kuwakumbatia baadhi ya mabinti alijikuta akilia.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad