Rais wa Urusi Vladimir Putin Aionya Marekani...."Tupige, Tuwapige''

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais wa Urusi Vladimir Putin Aionya Marekani...."Tupige, Tuwapige
Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameahidi kuzifuatilia kwa karibu hatua za Marekani zilizotangazwa na Rais Donald Trump kuhusu mpango wa kujenga upya vinu vya silaha zake za kinyuklia.

Putin amezungumzia hatua hizo za Marekani baada ya Trump kutishia kuachana na mpango wa makubaliano ya udhibiti wa makombora yenye uwezo wa kupiga maeneo nyeti ya Ulaya, uliosainiwa mwaka 1987 kati ya viongozi wa dola ya Kisoviet na Marekani, maarufu kama ‘INF treaty’.

Rais huyo wa Urusi ameonya nchi za bara la Ulaya kuwa zitakuwa kwenye hatari ya mstari wa mapambano kama Marekani na Urusi zitafutilia mbali makubaliano hayo ya mwaka 1987.

Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita alipoalikwa kama mgeni rasmi kwenye mjadala wa Valdai, Putin alisisitiza kuwa Urusi haimuogopi mtu yeyote wala nchi yeyote.

Hata hivyo, alisisitiza kuwa nchi yake haitaanzisha mashambulizi kwa nchi yeyote lakini ikipigwa itajibu kwa kipigo kikali zaidi. “Tupige, tukupige,” anakaririwa.

Akifafanua kauli yake, aliweka ucheshi kuwa muathirika wa kipigo hicho cha majibu hatakuwa na muda wa kutubu kwani kipigo kitampeleka moja kwa moja kaburini.

Mwaka jana, Trump amewahi kukaririwa akionya kuwa hakuna atakayesalimika katika vita ya makombora ya nyuklia kati ya nchi yake na Marekani.

“Sidhani kama kuna atakayesalimika kwenye mgogoro huo wa kinyuklia,” alisema Putin. “Lakini kuna matumaini ya utulivu kwetu wakati wote, hadi itakapofikia hatua ya kutusukuma na kuwa tayari kutuzika,” aliongeza.

Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya kivita wamekaririwa na BBC kuwa mgogoro huo utabaki kuwa katika kauli za viongozi na hautakuwa na madhara ya hatua za kweli za kijeshi, kwani kauli hizo na uhusiano wa nchi hasimu pamoja na washirika wao haujafikia hata robo ya joto la vita baridi.

Imeripotiwa kuwa Putin na Trump wanaweza kukutana hivi karibuni jijini Paris nchini Ufaransa kuzungumzia joto la mkataba wa INF.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad