Makonda ajibu kuhusu matumizi mabaya ya mamlaka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Makonda ajibu kuhusu matumizi mabaya ya mamlaka
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amepinga moja ya hoja zilizotolewa na wahudhuriaji wa kongamano hilo, ikiwemo hoja iliyosema kwamba alidai asilimia kubwa ya wateule wa Rais wamekuwa wakitumia vibaya mamlaka yao.


Akichangia kwenye kongamano hilo Makonda amesema kuwa idadi kubwa ya watu wanaolalamika matumizi mabaya ya wateule hao wa Rais walikuwa wanufaika wa mfumo mbovu.

“Rais hajamtuma RC na DC kutumia mamlaka vibaya, kupima utendaji wa Rais Magufuli ni kama kutoa treni barabarani kuirudisha kwenye reli, kwa hiyo lazima kuna vyuma lazima vitalalamika, niwaombe tusichukulie matukio machache yanatokea kuwa ni maagizo ya Rais”, amesema Paul Makonda.

Awali Mbunge mteule wa Jimbo la Ukonga jijini Dar es salaam, Mwita Waitara amemshauri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kuangalia upya namna ya kuzalisha ajira kwa vijana ili kupunguza vilio vya ajira.

Akichangia kwenye kongamano la kujadili hali ya uchumi na siasa katika kipindi cha miaka 3 cha serikali ya awamu tano, Waitara amesema suala la ajira kwa wananchi wa Tanzania lipewe kipaumbele.

“Nikushauri mheshimiwa Rais kuna shida ya ajira Tanzania awaombe wasaidizi wake, wazalishe ajira nchini hasa kwa vijana, vijana wengi nchini na vijana wanatumika kisiasa naomba ajira itafutwe ili waweze kuishi”, amesema.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad