Mume Amuuwa Mkewe kwa Kumpiga na Jiwe

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mume Amuuwa Mkewe kwa Kumpiga na Jiwe
MFANYAKAZI wa shsirika la simu nchini (TTCL) mkoani wa Shinyanga aitwaye Bupe Jacob maarufu kwa jina la Mwakibibi (48) ameuawa kwa kupigwa jiwe kichwani na mume wake aitwaye Shyrock Kimaro (48) mwendesha bodaboda mkazi wa Ibadakuli mjini Shinyanga.
fb_img_1541511268309-jpeg.923932
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Alchelaus Mutalemwa,  tukio hilo limetokea Novemba 5, 2018 majira ya saa 12 jioni katika Mtaa wa Miti Mirefu, Kata ya Mjini, Manispaa 
ya Shinyanga.

Amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi baina ya Shyrock na mkewe Bupe ambao walitengana hivi karibuni.

“Siku ya tukio Bupe alimpigia simu mme wake akiomba pesa za matumizi ya mtoto lakini katika kutoelewana walianza  kujibizana na kusukumana ambapo Bupe akaanguka chini.  Mme aliyekuwa amelewa akachukua jiwe na kumpiga mkewe kichwani akafariki dunia,” amesema Kamanda Mutalemwa akiongeza polisi inamshikilia mtuhumiwa na atafikishwa mahakamani.





----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad