Paula Akizingua Namfundisha Adabu- Kajala

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Paula Akizingua Namfundisha Adabu- Kajala
KARIBU mpenzi msomaji ndani ya safu hii mpya kabisa ya Staa na Familia. Hapa tutakuwa tunakuletea mastaa mbalimbali ambao wamejaliwa kupata watoto. Watapata nafasi ya kueleza furaha na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wanapokuwa na watoto wao.

Kwa kuanzia tunaye staa mkubwa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’. Anaeleza ni jinsi gani anavyoishi na mtoto wake, Paula Paul mwenye umri wa miaka 16 ambaye amezaa na prodyuza maarufu Bongo, Paul Matthysse ‘P Funk’ ambaye amemaliza darasa la saba mwaka huu katika Shule ya Sunrise iliyopo Kinondoni, Dar. Kajala amefunguka maisha yake na mtoto wake huyo kama ifuatavyo;

ANAISHIJE NA MTOTO WAKE HUYO?

Kajala: “Wengine hawawezi kujua ni jinsi gani ninaishi na Paula. Unajua mimi ni mama kijana, lakini lazima mtoto wangu anitii na aishi vile ninavyotaka au ninavyomuelekeza na akinizingua ninamfundisha adabu.

“Lakini pia kuna wakati tunaweza kuzungumza tukacheka na kutaniana.”

ANAMPIGA AKIMKOSEA?

Kajala: “Tena siyo kitoto, anaponikosea mimi ni mkali sana. Siku zote nilifundishwa na mama yangu ‘akupigaye ndiye anayekufunza’. Paula anapokosea ninamfundisha na panapostahili kumchapa nafanya hivyo japokuwa siyo mara nyingi maana Paula ni mkubwa sasa, tunakaa tunazungumza na ananielewa vizuri na kuna kipindi tunakuwa marafiki sana.”

VIPI KUHUSU MALEZI YA KWAKE MWENYEWE BILA BABA?

Kajala: “Ni magumu kwa sababu sidhani kama kuna mama anapenda kulea mtoto bila baba ila kwa sababu imenilazimu kuwa hivyo, sina jinsi na uzuri Mungu kanipa nguvu ya kusimama kama mama ingawa huwa anakwenda kwa baba yake anapopata nafasi.”

VIPI KUMVALISHA MAVAZI YA KIMJINI?

Kajala: “Sidhani kama kuna nguo ya ajabu ambayo ninamvalisha Paula, lakini najaribu kumuweka mtoto wangu kisasa zaidi na sidhani kama mavazi yanaweza kufanya tofauti au kumbadilisha tabia maana ninamkuza ili vitu vingine aone vya kawaida tu.”

KWA NINI HAPENDI KUONGOZANA NAYE?

Kajala: “Nafikiri siyo sahihi sana kila sehemu niende na mtoto wangu, si vizuri ajue kila kitu anachofanya mama yake, kuna mipaka yake, kuna sehemu ninapaswa kuwa naye, tukae tule, aogelee na mambo mengine…”

ANAMCHUKULIAJE PAULA?

Kajala: “Paula ni roho yangu kabisa, ninampenda mno na ni mtoto ambaye amenifundisha maisha vilivyo na pia ni mtoto wa historia ya maisha yangu.”
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad