Shilole Aamia Nyumbani Kweke na Bonge la Mkosi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Shilole Aamia Nyumbani Kweke na Bonge la Mkosi
MWANAMAMA ambaye ni staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, wiki iliyopita alihamia kwenye mjengo wake mpya uliopo Majohe, Gongo la Mboto jijini Dar, lakini akapata mkosi kufuatia kuanguka na kupasuka usoni.  Akizungumza na Ijumaa Wikienda akiwa na nundu kwenye paji la uso ndani ya Ukumbi wa Next Door Arena uliopo Masaki jijini Dar ambako kulikuwa na bethidei ya msanii wa Bongo Fleva, Faustina Charles ‘Nandy’, Shilole alifunguka mkasa mzima.

Akiwa kwenye pati hiyo, Shilole alionekana akiwa amekaa na wasanii wenzake wa kike, Mwasiti Almas na Esterlina Sanga ‘Linah’ huku akiwa na nundu usoni na mdomo wake ukiwa umechanika sehemu ya juu.

Baada ya kuona hali hiyo huku kukiwa na minong’ono kuwa huenda alipigwa na mumewe, Ashraf Uchebe, Ijumaa Wikienda lilimsogelea Shilole na kumuuliza kuliko au kuna masahibu gani yaliyomkuta ambapo alifunguka:“Aaa…Unajua juzijuzi ndiyo nimehamia nyumbani kwangu Majohe, sasa nyumba yenyewe bado sijaizoea na bado sijaweka umeme, sasa niliporudi usiku nikiwa nimechoka ndiyo nikajikuta napiga mwereka na kuumia hivi.

“Si unajua nyumba usiyoizoea? Hayo ndiyo yaliyonikuta na hii pati kwa kuwa nilishaalikwa na kumhakikishia Nandy kuwa nitakuwepo, nimeona nijikongoje nifike haina jinsi.”

Hata hivyo, licha ya kuwa na majeraha hayo, Shilole alionekana kuwa mchangamfu kama kawaida yake na kuvamia sehemu ya kuchezea kisha akatoa machejo wakati akibanjuka na kuwafanya wageni waalikwa kupiga mayowe ya kumshangilia
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad