Shetta afunguka kuhusu kutengeneza umaarufu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Shetta afunguka kuhusu kutengeneza umaarufu
Staa wa Bongofleva Shetta ameibuka na kuiambia eNEWZ kwamba, umaarufu wa mtoto wake sio wa kutengeneza kama mastaa wengine wanavyofanya kwa watoto wao bali wa mtoto wake Qayllah umejitengeneza wenyewe kutokana na watu kumkubali mambo anayofanya.

Akiongea kupitia eNEWZ Shetta amesema umaarufu ambao mtoto wake anao mpaka sasa hajahusika hata kidogo kuutengeneza kwa maana hajawahi kutumia muda wake mwingi kumtangaza wala kumfanyia mtoto wake kitu chochote ambacho kingefanya jamii imfahamu au kufatilia kile anachokifanya.

 "Kwa kweli umaarufu wa mwanangu Qayllah hata mimi mwenyewe unanishangaza kwa maana kila siku zinavyozidi kwenda nashangaa anafanya vitu ambavyo vinafanya watu wazidi kumpenda, yaani mpaka sasa naona kama anataka kuzidi jina la Shetta sasa maana watu wananiita baba Qayllah badala ya jina langu"aliongea Shetta.

Hata hivyo Shetta hakusita kutoa ufafanuzi juu ya nani mmiliki wa Band ya The Mafik baada ya wasanii wa  Band hiyo kukana  kwamba Shetta sio mmiliki wao, nakusema yeye kwa sasa ana hisa kwenye kampuni ya King Empire na ana cheo ambacho kinamfanya kumiliki kila kitu kilichopo ndani ya kampuni hiyo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad