Sugu apandisha dau kwa mtu mwenye picha yake

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sugu apandisha dau kwa mtu mwenye picha yake
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu', ametangaza kuongeza kitita cha shilingi milioni 5 kwa mtu yeyote atakayebahatika kuwa na picha yake wakati akiwa gerezani kwa kile alichokidai mpaka sasa hakuna aliyejitokeza na picha hiyo.


Maamuzi hayo ya Sugu yanakuja baada ya awali kutangaza kitita cha shilingi milioni 1 kwa atakayepata picha yake ili aweze, kukamilisha kitabu chake ambacho anatarajia kukitoa baada ya kupatikana kwa picha hiyo.

“Ni kweli mpaka sasa hakuna aliyejitokeza kuonesha picha halisi nikiwa gerezani, wengine wanakuja na picha ambazo zimetengenezwa, wengine wanaleta nilipokuwa mahakamani, kwa hiyo tumeona tupandishe  dau.”

“Timu yangu  inahangaika na ndiyo  maana tumetangaza kuanzia milioni  3 hadi milioni 5, kwa hiyo nasisitiza atakayeipata atuletee, mara moja ili nikamilishe kitabu changu,” ameongeza Sugu.

Sugu alifungwa katika gereza la Ruanda Jijini Mbeya akitumikia kifungo cha miezi (5) baada ya kukutwa na hatia ya kutoa lugha ya kashfa dhidi ya Rais Magufuli ambapo hukumu yake ilitolewa Februari 26, 2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Michael Mteite. Mh Joseph Mbilinyi (SUGU) aliachiliwa huru Mei 10.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad