Vanessa Mdee Aanika Ugumu Alioupata Kuimba Kihindi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Vanessa Mdee Aanika Ugumu Alioupata Kuimba Kihindi
STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘Vee Money’ ameanika ugumu alioupata wakati wa kuimba wimbo wa lugha ya Kihindi unaoitwa ‘Vaishnav Jan’.



Vee Money aliiambia Risasi Vibes kuwa, alifuatwa na ubalozi wa India ambao upo Tanzania ili autunge na kuuimba wimbo huo kwa ajili ya kutumika kwenye maadhimisho ya miaka 150 ya kufariki kwa baba yao wa Taifa, Mahatma Gandhi ambayo hufanyika kila mwezi Oktoba huko India.



“Orijino wa wimbo huu umefanywa na msanii wa kwao wa zamani sana wa kike, sasa katika kuadhimisha miaka hiyo 150 wakaona watafute mtu mbadala wa kufanya kava kwa ajili ya kucheza pamoja na video ndipo wakanipata mimi,” alisema Vee Money na kuongeza;



“Kwa hiyo kutokana na fursa hiyo nikafanya wimbo nikiongoza na mwalimu wa lugha ya Kihindi na tukashuti video ndogo ambayo ipo Youtube.



Ilikuwa kazi kwani Kihindi sijui lolote hata ukinitukana lakini kwenye kuimba nimefanya vizuri na tayari nimepokea barua kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje India, Swaraj akinipongeza kwa kazi nzuri niliyoifanya.”
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad