Buju Apokelewa Kifalme Jamaica Baada ya Kumaliza Kifungo Marekani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Buju Apokelewa Kifalme Jamaica Baada ya Kumaliza Kifungo Marekani
Wasanii nchini Jamaica wameonesha kuwa na furaha kubwa wakimkaribisha nyumbani msanii mwenzao mkongwe kwenye muziki wa reggae nchini humo, Buju Banton, ambaye alikuwa kifungoni nchini Marekani.


Wasanii hao wametumia mitandao yao ya kijamii kuonesha furaha iliyopo mioyoni mwao, baada ya Buju Banton ambaye jina lake halisi ni Mark Anthony Myrie kuachiwa huru kutoka kifungoni.

Buju Banton ambaye ni maarufu kwenye muziki wa reggae akiwa na nyimbo kadhaa maarufu kama Destiny, Its not easy road, Un told stories na nyinginezo, alifungwa nchini Marekani katika jimbo la Georgia, mwaka 2011 kwa makosa ya kusafirisha madawa ya kulevya.

Desemba 7 mwaka huu, msanii huyo aliachiwa huru baada ya kumaliza kifungo chake, na kuudi nyumbani Jamaica, ambako alipokelewa kwa furaha kubwa na wasanii wenzake.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad